Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, katika ziara fupi za kuangalia pembejeo za ruzuku za zao la korosho |
Na Juma Mohamed, Tandahimba.
MAWAKALA wa
ugawaji wa pembejeo za zao la korosho nchini wametakiwa kutenda haki kwa
wakulima na kuacha kufanya kazi hiyo kwa ajili ya masilahi yao na atakaefanya
hivyo serikali itawachukulia hatua kali ikiwemo kuwafilisi mali zao na
kuwafunga.
Hayo
yameelezwa na mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, wakati wa uzinduzi wa ugawaji
na uhamasishaji wa pembejeo za ruzuku za zao la korosho msimu wa kilimo wa
2016/2017, uliofanyika wilayani Tandahimba, na kusema kuwa mawakala hao
wanakwepa kufanya kazi na serikali za vijiji.
Halima Dendego |
“Serikali ya
kijiji ndio yenye watu, uongo kweli? Ndio yenye wakulima, uongo kweli?..leo
wakala unasema hutaki kufanya kazi na serikali ya kijiji inamaana una watu wako
kwenye mfuko unaotaka kuwapa pembejeo zetu za ruzuku, hatuta kubali kama kazi
hii imekushinda ni hiyari, hacha wenyewe tutaifanya..” alisema.
Alisema,
wakala atakaekwenda kinyume na matakwa ya serikali kwa kuuza pembejeo za ruzuku
kwa bei anayotaka mwenyewe na hata ikibainika pembejeo hizo kuuzwa katika
maduka kwa bei ya soko, utafilisiwa na kufungwa.
“Kwahiyo
nitoe tahadhari kwa mawakala nchi nzima, mchezo wa kucheza na wakulima wetu uwe
mwisho..” aliongeza.
Aidha,
aliwataka wadau wa zao hilo kushirikiana na viongozi wa Bodi ya Korosho ya
Korosho Tanzania (CBT), na viongozi wa serikali katika kuwapiga vita watu
wachache wanaosambaza propaganda kuwaaminisha wakulima kuwa mfumo wa stakabadhi
ghalani haufai.
Alisema,
mfumo huo una manufaa makubwa kwa wakulima na ndio maana wataalamu wa zao hilo
wameuamini ambapo kuna baadhi ya watendaji ndio wanataka kuuharibu hivyo
jitihada za dhati zinahitajika kuweza kupambana nao.
Alisisitiza
kwa mikoa na wilaya zinazolima zao hilo kujitahidi kuhamasisha mfumo huo ambao
mkoa wa Pwani tayari wakulima wake wamehamasika kwa kiasi kikubwa kuutumia na
kuona mafanikio yake.
Naye,
mwenyekiti wa Bodi hiyo, Anna Abdallah, alisisitiza kwa wakulima kutekeleza
agizo la waziri mkuu wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa,
la kuvitaka vijiji kupanda miche 5,000 na kila kaya angalau walime heka moja ya
korosho.
No comments:
Post a Comment