Bryson Raphael akishangilia goli la kwanza la Ndanda alilofunga dhidi ya Mwadui. |
wachezaji wa Ndanda wakishangilia goli la pili. |
Wzungu wakiwa wamejinganya na mashabiki wenzao wa Ndanda kuishangilia timu yao. |
Wachezaji wa Ndanda, Atupele Green, Ahmad Msumi na Kigi Makassy wakishangilia bao la pili na la ushindi lililofungwa na Msumi dakika za majeruhi katika mechi ya ligi kuu dhidi ya Mwadui. |
William Lucian na Kigi Makassy wakishangilia bao la pili. |
Salum Minelly wa Ndanda akimiliki mpira mbele ya Juma Mnyasa wa Mwadui. |
Na Juma Mohamed, Mtwara.
Timu ya soka
ya Ndanda Fc ya mkoani Mtwara imeendelea kujihakikishia kubaki katika ligi kuu
ya Tanzania bara, baada yah ii leo kufanikiwa kufikisha pointi 30 katika
msimamo kwa kuifunga Mwadui Fc ya Shinyanga kwa mabao 2-1 katika mchezo
uliofanyika uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
Mabao ya
washindi yalifungwa na Bryson Raphael katika dakika 29 baada ya kuachia shuti
kali la nje ya 18 lililomshinda mlinda mlango Shabani Kado na Ahmad Msumi
aliyefunga bao la ushindi dakika ya 90 kwa kuunganisha krosi ya Atupele Green,
huku bao la kufutia machozi la Mwadui likifungwa na Kelvin kongwe dakika ya 61
baada ya kuwatoka walinzi wa Ndanda waliodhani kuwa ameotea.
Bryson Raphael akishangilia goli la kwanza la Ndanda alilofunga dhidi ya Mwadui. |
Kocha wa
Mwadui, Jamuhuri Kiwelo amesema timu zote zimecheza vizuri lakini Ndanda
waliweza kutimia vizuri nafasi walizozipata na kuweza kupata ushindi huo na
kudai kuwa goli la pili lilitokana na nafasi ambayo ilipotezwa na Mwadui
langoni mwa Ndanda.
“Ukifanya
makosa utafungwa ukicheza vizuri utafungwa, nafikiri nafasi walioipata wale ilikuwa
tufunge sisi baada ya kukosa attempt ile ikahamia kwetu tumefungwa goli, lakini
game ilikuwa nzuri na timu zote zilicheza vizuri..hao walikuwa wanataka point
Tatu wsogee juu kutokana na position waliokuwa nayo na sisi tulikuwa tunataka
point Tatu ili tujiweke juu katika nafasi nzuri ya kumaliza nafasi ya Nne..”
alisema Julio.
Shangwe |
Naye, kocha
msaidizi wa Ndanda, Mussa Mbaya, amesema pamoja na timu yake kuonekana kupata
matokeo mazuri kwa baadhi ya mechi zake katika kuelekea mwisho wa ligi, lakini
bado anahitaji kushinda zaidi ili ajihakikishie kubaki katika ligi, huku
akiwasifu wachezaji wake kwa kucheza kwa kutokata tamaa na kuweza upata goli
dakika za mwisho.
“Nafikiri ni
spirit kwasababu mchezaji kama yuko fiti hawezi kkata tama mpka dakika 90
atapambana, mimi nafikiri wachezaji wako vizuri wana mazoezi ya kutosha na ndio
maana wanaweza kupambana mpaka mwisho wa mchezo..Mwadui ni timu nzuri na kule
kwao walitufunga matokeo kama haya ya goli 2-1 na sisi leo tukasema haiwezekani
mpaka dakika Tatu za nyongeza tukaweza kupata bao..” alisema.
Wachezaji wa Ndanda wakifurahia goli. |
Ahadi ambayo
ilitolewa na Mbunge wa Tandahimba (CUF) Mhe. Katan Ahmad, iliendelea
kutekelezwa baada ya kuwakabidhi viongozi wa Ndanda fedha kiasi cha sh. Milioni
1.4 ambazo ni za ushindi kwa timu na idadi ya magoli yaliofungwa.
Matokeo kama
hayo waliwahi kuyapata Mwadui katika mchezo wa mzunguko wa kwanza dhidi ya
Ndanda katika mchezo uliozechezwa Shinyanga.
Baada ya
matokeo ya leo, Ndanda wamesogea mpaka nafasi ya Nane katika msimamo wakiwa na
points 30 baada ya kucheza mara 26, huku Mwadui wakisalia katika nafasi ya Sita
kwa points zao 34 baada ya kucha mara 25.
Mchezo ujao
Ndanda watacheza na Kagera Sugar katika uwanja wa Nangwanda Sijaona, mchezo
ambao utachezwa Aprili 16 mwaka huu, huku Mwadui wakiwafuata Yanga katika
mchezo utakaopigwa katika uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Matokeo ya michezo mingine ya leo VPL ni:
Afican
Sports 1-0 Kagera Sugar
Mtibwa Sugar
1-1 Prisons
CAF Champions League:
Yanga 1-1 Al
Ahly.
No comments:
Post a Comment