Mbunge wa Mtwara mjini (CUF) Maftaha Nachuma, akiwahutubia wananchi wa Mtwara mjini walijitokeza katika uwanja wa Mashujaa kumsikiliza katika mkutano wa kuwapongeza kwa kumchagua kuwa mbunge |
Mbunge wa Mtwara mjini (CUF) Maftaha Nachuma, akiwahutubia wananchi wa Mtwara mjini walijitokeza katika uwanja wa Mashujaa kumsikiliza katika mkutano wa kuwapongeza kwa kumchagua kuwa mbunge |
Wananchi waliojitokeza katika uwanja wa Mashujaa mjini Mtwara kwa ajili ya kumsikiliza Mbunge wao Maftaha Nachuma (CUF) ambaye alifanya mkutano wa kuwapongeza kwa kumchagua kuwa mbunge |
Na Juma Mohamed, Mtwara.
MBUNGE wa
Mtwara mjini kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Maftaha Nachuma, amepingana na
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) juu ya mikoa ya Mtwara na Lindi
kuwepo katika mradi wa kusambaza gesi majumbani unaotarajiwa kutekelezwa na
shirika hilo.
Akizungumza
katika mkutano wa hadhara wa kuwapongeza wananchi kwa kumchagua kuwa mbunge
ulioambatana na zoezi la kutambulisha magari ya kubebea wanafunzi katika uwanja
wa Mashujaa mjini hapa, alisema amepitia mpango wa shirika hilo na kujiridhisha
kuwa mikoa hiyo haipo katika mradi huo.
Hotuba |
Alisema,
katika mpango wa mwaka 2016/2017 wa TPDC unaonesha mkakati wao wa kuongeza
megawati za umeme ambazo zitatumika Tanzania nzima kupitia mradi wa bomba la
gesi linalotoka Madimba mpaka Kinyerezi, Dar es Salaam lakini katika mpango wa
pili ambao ni wa kusambaza gesi majumbani mikoa hiyo haipo.
“Lakini cha
ajabu katika mpango wa serikali ndugu zangu pamoja na kwamba huu mkakati na
utekelezaji unaanza baada ya bajeti ya mwezi wa saba mwaka huu, kusambaza
mabomba ya gesi majumbani, Mtwara na Lindi ambako gesi inatoka, haipo ndugu
zangu..Mtwara na Lindi inakotoka gesi kwenye ule mpango haijawekwa kwamba
wanamtwara na sisi tuweze kutumia gesi kwa ajili ya kupikia na mambo mengine
tuhepukane na kuni haijawekwa ndugu zangu ni mambo ya kusikitisha kwakweli..”
alisema.
Nyomi |
Hata hivyo,
kauli hiyo ya Mbunge inapingana na maelezo yaliyotolewa na mkurugenzi mtendaji
wa shirika hilo, James Mataragio, ambayo alimweleza Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, alipofanya ziara katika kiwanda cha
kuchakata gesi asilia cha Madimba mkoani hapa Februari 27 mwaka huu kwamba “Miradi
mingine inayotarajiwa kutekelezwa na TPDC ni pamoja na mradi wa uagizaji wa
mafuta ya hifadhi ya taifa, mradi wa usambazaji gesi majumbani katika mikoa ya
Lindi, Mtwara na Dar es Salaam..”.
Mbali na
maelezo hayo ya mkurugenzi, Meneja wa biashara ya gesi wa shirika hilo, Emmanuel
Gilbert, aliwahi kuwaeleza waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa semina
ya siku moja kwa waandishi juu ya kuwajengea uwezo wa masuala ya mafuta na
gesi, kuwa shirika lipo katika mchakato wa ujenzi wa mradi huo na kwamba tayari
upembuzi ya kinifu katika mikoa ya Lindi na Mtwara umekamilika.
Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, akiongea jambo na mkurugenzi mtendaji wa TPDC, James Mataragio. |
Alisema,
mradi huo ambao utatekelezwa katika mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara na Lindi kwa
sasa zinasubiriwa fedha kutoka serikalini kwa ajili ya kuanza zoezi la usanifu
wa michoro katika maeneo yatakayopitiwa na miundombinu hiyo.
Kwa mujibu
wa Gilbert, mtandao wa kutandaza mabomba wa mradi huo utakuwa na urefu wa Km 17
kwa mkoa wa Mtwara ambapo unatarajiwa kuunganisha nyumba 11,000 na magari 4,000
ambayo yatakuwa na yanauwezo wa kuamua kutumia nishati ya gesi au mafuta, na Km
11 kwa mkoa wa Lindi.
Mabasi aina ya Toyota Coaster ambayo yamenunuliwa na Mbunge wa Mtwara mjini (CUF) Maftaha Nachuma, kwa ajili ya kubebea wanafunzi kuwapeleka shule na kuwarudisha. |
No comments:
Post a Comment