Friday, September 4, 2015

Walezi Simba na Yanga kuzindua 'KiliFest'


Kilifasta
Bia ya Kilimanjaro Premium Lager imezindua rasmi tamasha maalumu linalojulikana kama ‘KiliFest’ ambalo litakuwa la aina yake na la kwanza kuwahi kuandaliwa Tanzania.
Tamasha hilo lilizinduliwa Jijini Dar es Salaam Alhamisi Septemba 3, 2015 na linatarajiwa kufanyika JUmamosi Septemba 26, 2015 katika Viwanja vya Leaders Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Meneja wa Kilimanjaro Premium Lager, Pamela Kikuli alisema lengo ni kuleta kwa watanzania kitu cha aina yake ambacho kitabaki katika kumbukumbu zao na pia itawaleta karibu zaidi na bia yao namba moja.
“KiliFest ni tamasha la aina yake na halijawahi kutokea Tanzania ni matumaini yetu kuwa watanzania watajitokeza kwa wingi katika viwanja vya Leaders ili wawe sehemu ya tukio hili la aina yake,” alisema.
Alisema milango ya Leaders itafunguliwa saa nne kamili na kutakuwa na matukio mengi ya kufurahisha na kuburudisha kama vile michezo, chakula, vinywaji, changamoto mbalimbali, burudani na zawadi nyingi pia zitatolewa na kuongeza kuwa vyakula mbali mbali na vinywaji vitauzwa.
“Wote watakaohudhuria watapata kitu cha kuwafurahisha na tumeandaa tamasha hili kwa namna ambayo shughuli hazitasimama hata kwa dakika moja kuanzia mwanzo hadi mwisho,” alisisitiza.
Kwa mujibu wa Meneja huyo, tiketi za tamasha hilo zitauzwa katika maeneo mbalimbali kama itakavyotangazwa baadaye katika redio na zitauzwa elfu 10 na akatoa wito kwa wote wanaotaka kuhudhuria kuhakikisha wanajipatia tiketi zao mapema kuepuka usumbufu wa foleni kubwa dakika za mwisho.
Aliwataja baadhi ya wasanii ambao watatoa sehemu ya burudani wakati wa tamasha hilo ambao ni pamoja na Mapacha Watatu, Maua, Ruby, Damian Soul, Vanessa Mdee, Ben POl, Weusi, Fid Q, Isha Mashauzi na Shettah.
Wasanii waliohudhuria katika uzinduzi huu ni pamoja na Ruby, Shettah, Ban Pol, Nick wa pili na G-Nako.
“Baadhi ya watakaohudhuria watapata nafasi ya huduma zenye hadhi ya juu (VIP) baada ya kushiriki katika matukio mabalimbali ya siku hiyo na kushinda na kwa kweli watafurahia,” alisema.
Alisema tamasha hili liko wazi pia kwa wakazi wa mikoani na kwao hili litakuwa tamasha la aina yake na hawatakuwa wanapoteza muda kusafiri na kuwa sehemu ya tamasha hilo.
Aliendelea kusema kuwa Bia ya Kilimanjaro ni maarufu kwa burudani, mpira na riadha sasa inaleta sokoni kitu cha aina yake ambacho ni cha kusisimua zaidi kama njia ya kuwazawadia wateja wake kwa kuwaandalia tukio la aina yake ambalo litawaacha wakitamani zaidi.
Kilimanjaro Premium Lager ndio mdhamini mkuu wa Tuzo za Muziki Tanzania (KTMA), Mbio za Kilimanjaro maarufu kama Kilimanjaro Marathon. Timu ya Taifa (Taifa Stars) na vilabu vya Simba na Yanga.
SOURCE: KILI WEBSITE

No comments: