Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari |
Hayo yamezungumzwa na
msemaji wake, Garba Shehu, na kwamba kiasi hicho kinaonyesha kuwa amekuwa
akiishi “maisha ya kujinyima”,
Bw
Buhari anamiliki makao matano na nyumba mbili za matope, pamoja na mashamba
kadha, akaongeza.
Kiongozi huyo wa zamani wa
kijeshi alichaguliwa kuwa rais mwezi Machi ahadi zake kuu zikiwa kukabiliana na
ufisadi na ukosefu wa usalama.
Ufisadi ni tatizo sugu
katika taifa hilo lenye uchumi mkubwa barani Afrika na mwezi uliopita, Bw
Buhari alisema $150bn (£100bn) zimeporwa kutoka kwa hazina ya serikali.
Bw Shehu alisema kupitia
taarifa kuwa Bw Buhari ana shamba la matunda na renchi yenye ng’ombe 270,
kondoo 25, farasi watano na ndege wengi.
Pia anamiliki hisa katika
kampuni tatu - Berger Paints, Union Bank na Skye Bank, taarifa hiyo iliongeza.
Hata hivyo, makamu wa rais
wa Nigeria Yemi Osinbajo ni tajiri kumshinda mdosi wake.
Taarifa hiyo ilisema Bw
Osinbajo ana $900,000 (£600,000) kwenye akaunti zake za benki.
Kwenye fomu ya kutangaza
utajiri wake, Bw Osinbajo pia alifichua anamiliki nyumba nne, moja ikiwa ya vyumba
viwili vya kulala ambayo analipia mkopo mjini Bedford, Uingereza.
Taarifa hiyo haikusema
thamani halisi ya mali yote ya rais na makamu wake, ikieleza kuwa stakabadhi
zilizokabidhiwa Afisi ya Maadili zitafanywa wazi kwa umma karibuni baada ya
ukaguzi wake kukamilika.
SOURCE: BBC
No comments:
Post a Comment