Mashabiki waliojitokeza kushuhudia mchezo kati ya Ndanda Sc na Azam Fc |
Jukwaa kuu |
Waandishi wa habari wakifanya yao |
Na Juma Mohamed, Mtwara.
Mechi ya
kirafiki ya kuadhimisha siku ya Ndanda (Ndanda Day) iliyopigwa leo katika
uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara, kati ya wenyeji Ndanda Sc dhidi ya
wanalambalamba Azam Fc, imemalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1, kwa mabao ya
Kelvin Friday kwa upande Azam kabla ya Omari Nyenje kuisawazishia Ndanda Sc kwa
kichwa.
Akizungumza baada
ya mchezo huo, kocha wa timu ya Ndanda, Hamimu Mawazo, amesema bado
hajaridhishwa na kiwango cha wachezaji wake hivyo kazi ya ziada inahitajika ili
kuweza kuwaweka sawa kabla ya kuanza mikikimikiki ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Kwa upande
wake, kocha wa Azam Fc ambao walishusha kikosi B na baadhi ya wachezaji wa
kikosi cha kwanza kutokana na makubaliano baina yao na Ndanda, Benis Kitambi,
amesema mchezo ulikuwa mzuri na kwamba wao waliuchukulia kama mchezo wa
kuwapima wachezaji wao ili waeze kupata uzoefu.
Katika mchezo huo, mlinzi wa Azam, David Mwantika, alijikuta akitolewa nje kwa kuonyeshwa kadi nyekundu baada ya kumchezea madhambi mshambuliaji wa Ndanda Omari Nyenje, aliekuwa akielekea golini akibaki yeye na golikipa, ambapo Ndanda walipata penaiti iliyopigwa na Kigi Makasy ambaye hata hivyo alipaisha.
Watoto wakiimba na kucheza nyimbo za kuishangilia timu yao ya Ndanda Sc. |
Aidha,
mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Mtwara, Athumani Kambi, amesema,
wameshindwa kufikia lengo katika mchezo huo ambao ulikuwa maalumu kwa ajili ya
kuwatambulisha wachezaji wapya kwa mashabiki na kuchangisha fedha za kuisaidia
timu hiyo, kutokana na uchache wa mashabiki waliojitokeza.
No comments:
Post a Comment