Sunday, July 15, 2012

SIMBA YAPIGWA KAMA YANGA, AZAM YAANZA SARE CHAMAZI

URA ya Uganda imeichapa Simba SC mabao 2-0, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, katika mechi ya Kundi A, Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
URA ilipata mabao yake kupitia kwa Owen Kasuule dakika ya 11 Feni Ally dakika ya 90+2.
Katika mchezo huo, Simba ilicheza vizuri, lakini tu walishindwa kutumia vizuri nafasi walizopata na mabao yote walifungwa wakitoka wao kushambulia.
Kikwazo kwa Simba leo alikuwa ni beki Derrick Walullya ambaye msimu uliopita alichezea Simba, akatemwa kwa madai kiwango kimeshuka. Aliwatia mfukoni washambuliaji wote wa Simba.
Katika Uwanja wa Chamazi, Azam FC wamelazimishwa sare ya 1-1 na Mafunzo, bao lao lililofungwa na John Bocco ‘Adebayor’dakika ya 26. Katika mchezo wa kwanza, Chamazi Vita Club imeifunga 7-0 Port ya Djibouti.
URA baada ya kupata bao la pili refa akiwazuia kushangilia muda mrefu warejee uwanjani kuendelea na mchezo

Mussa Mudde anatia krosi

Sunzu anapiga mishe

Feni Ally akishangilia baada ya kupiga la pili

Kipa wa URA, Mugabi Yassin akitibiwa baada ya kuumia katika harakati za kuokoa

Mugabi Yassin akidaka mbele ya Sunzu

Sunzu katika mishe mishe za kusaka mabao

Derrick Walullya akiondoka baada ya kumpokonya mpira Sunzu

Mugabi anadaka kiulaini

Sunzu baada ya kukosa bao la wazi

Sunzu anapiga, kipa anadaka

Timu zinaingia uwanjani

Benchi la Simba

Profesa Milovan na Msaidizi wake Hamatre

Kikosi kilichoanza Simba SC

Kikosi kilichoanza URA

Nahodha wa Simba, Juma Kaseja kushoto na Nahodha wa URA Massa Semeon wakisalimiana

Vikosi

Simba mashabiki

No comments: