Manji kulia akiteta na Sanga kushoto |
Zoezi la uchaguzi wa Yanga,
limekamilika na Yussuf Mehboob Manjia meshinda Uenyekiti wa klabu hiyo, wakati
Clement Sanga amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti na nafasi za Ujumbe Abdallah
Bin Kleb, Aaron Nyanda, Mussa Katabaro na George Manyama.
Nafasi ya Makamu Mwenyekiti
imekwenda kwa Clement Sanga aliyejipatia asilimia 62% ya kura zote zilizopigwa
katika nafasi ya u makamu mwenyekiti.
Akitangaza matokeo hayo,
majira ya saa 10:30 alfajiri katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Mwenyekiti wa
kamati ya uchaguzi wa klabu ya Yanga Jaji John Mkwawa amemtangza Manji kama
mishindi wa nafasi ya uenyekiti kufuatia kupata asilimia 97% ya kura zote
zilizopigwa katika nafasi hiyo.
Abdallah Bin Kleb, Moses
Katabaro, Aaron Nyanda na George Manyama wamechaguliwa katika nafasi ya ujumbe
wa kamati ya Utendaji.
Jaji Mkwawa amewashukuru wana
Yanga kwa kuwa wastaarabu na watulivu, kitu kilicholekea kufanyika uchaguzi kwa
amani na zoezi hilo kumalizika salama pasipo kuwa na rabsha yoyote.
Matokeo kamili ya wagombea
ni:
Nafasi ya
Mwenyekiti:
Yusuf Manji (kura 1876) 97.0%, John
Jembele (kura 40) 2.6%, Edgar
Chibura (kura 4) 0.24%
Nafasi ya Makamu
Mwenyekiti:
Clement Sanga (kura 1948) 62.6%, Yono
S Kevela (kura 475) 23%, Ayoub
Nyenzi (kura 288) 14%
Nafasi ya
Ujumbe:
Abdallah Bin Kleb (kura 1942), Moses Katabaro
(kura 1068), Aaron
Nyanda (kura
922), Geroge Manyama
(kura 682), Beda
Tindwa (kura
391), Edgar Fongo
(kura
295), Graticius
Ishengoma (kura 247), Jumanne
Mwamenywa (kura 251), Justine Baruti
(610), Lameck
Nyambaya (kura
425), Omary Ndula
(kura 170), Peter
Haule
(441), Ramadhan Said
(249), Yono Kivela
(123)
kutokana na matokeo yalivyo
hapo juu safu ya viongozi waliochaguliwa ni
Mwenyekiti: Yusuf
Manji,
Makamu
Mwenyekiti: Clement Sanga
Wajumbe:
Abdallah Bin Kleb, Moses Katabaro, Aaaron Nyanda, Geroge
Manyama
No comments:
Post a Comment