Tuesday, March 21, 2017

MAAFISA HABARI MIKOA YA MTWARA, LINDI NA RUVUMA WAKABILIWA NA UHABA WA VITENDEA KAZI.


Baadhi ya maafisa habari na maafisa TEHAMA wa mikoan ya Mtwara, Lindi na Ruvuma na halmashauri zake wakiwa katika mafunzo ya namna bora ya matumizi na uendeshwaji wa Tovuti za serikali kupitia mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma PS3 yanayoendeshwa na wizara ya Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI



JUMA MOHAMED, MTWARA

Baadhi ya maafisa habari wa halmashauri mbalimbali katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma wanakabilia na changamoto ya uhaba wa vitendea kazi kwa ajili ya kazi zao za kihabari, hali ambayo inapunguza ufanisi katika kazi.
Wakizungumza na Juma News katika semina ya kuwajengea uwezo maafisa habari wa mikoa hiyo, juu ya namna ya kuendesha tovuti za serikali kupitia mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma PS3, walisema kutokana changamoto hiyo wanalazimika kutumia simu kwa ajili ya kurekodi matukio, pale wanapokosa kuwa na kamera.
 “Tunajua ni changamoto kwa baadhi ya Halmashauri kukosa vifaa, lakini tunaweza kutumia njia ya kujiongeza kwa kutumia simu..simu za sasaivi zina mfumo wa Android, kwahiyo ukiwa na simu yenye Android unauwezo wa kurekodi Vidio vizuri na kuihariri..” alisema Teresia Malian, ambaye ni afisa habari halmashauri ya wilaya ya Tunduru.

Katibu tawala wa mkoa wa Mtwara Alfred Luanda akifungua mafunzo ya namna bora ya matumizi na uendeshwaji wa Tovuti za serikali kupitia mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma PS3 yanayoendeshwa na wizara ya Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI



Naye mtaalamu wa TEHAMA kutoka wizara ya TAMISEMI Edgar Mdemu, alieleza umuhimu wa Tovuti katika kuimarisha sekta za umma, kabla ya katibu tawala wa mkoa wa Mtwara Alfred Luanda, kusisitiza maafisa habari kuzingatia uzalendo katika kuchapisha habari zao kwenye tovuti hizo.
“Kwa kupitia hii ‘website framework’ basi naamini kwamba taarifa nyingi sana za halmashauri na mikoa zitakuwa kwenye ‘website’ kwa ajili ya wananchi kuweza kupata taarifa mbalimbali..” alisema Mdemu.
Semina hiyo inayojumuisha maafisa habari na maafisa TEHAMA wa halmashauri na mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma inatarajiwa kuhitimishwa Machi 27 mwaka huu.


No comments: