Wednesday, May 18, 2016

Madiwani Mikindani waitwa 'wanafiki' na wapiga kura wao.



Mmoja wa wakazi wa kata ya Jangwani tarafa ya Mikindani, akiwasilisha hoja zake kwa mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego (hayupo pichani) alipofanya kikao cha kazi na wakazi hao ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero zao.




Baadhi ya wanawake wa kata ya Jangwani tarafa ya Mikindani waliohudhuria kikao cha kazi kilichofanywa na mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego katika kata hiyo kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi.




Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, akipokelewa na wanawake wajasiliamali wa kata ya Jangwani tarafa ya Mikindani, alipokwenda kufanya kikao cha kazi kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi.


"Karibu mama yetu"


Na Juma Mohamed, Mtwara.

BAADHI ya wananchi wa Tarafa ya Mikindani mkoani hapa, wamewalalamikia madiwani wao kutoka vyama mbalimbali vya kisiasa kutokana na kutokuwa na umoja na nia ya kuwaletea maendeleo wananchi kwa madai kuwa hawana utaratibu wa kukutana kupanga mipango ya maendeleo kwa pamoja.
Akizungumza mbele ya mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima dendego, alipofanya kikao cha kazi na wakazi wa kata ya Jangwani katika tarafa hiyo, Ahmad Mkumilwa, aliwaita madiwani hao kuwa ni wanafiki na kwamba kama hataki kuwatumikia wananchi wao waliowachagua wajiuzulu.
“Tarafa ya Mikindani ina homa ya siasa, madiwani wote Chadema, CCM na CUF hawakutani wakapanga maendeleo ya Tarafa hii..kwahiyi ninachokuomba waambie kama tumewachagua kwa ajili ya kutupa maendeleo sisi waje vizuri, kama hawataki kutupa maendeleo sisi, wajiondoe mapema iwezekanavyo hatuwezi kukaa na wanafiki, maana ni wanafiki madiawani wa Mikindani, namwambia Lakshari (Diwani wa Jangwani) na yeyote Yule nakuambia wewe mkuu wa mkoa hawa ni wanafiki hawakutani..” alisema.
Alisema, afisa Tarafa anajitahidi kuitisha mikutano kwa ajili ya kujadili mambo ya 

Mmoja wa wakazi wa kata ya Jangwani tarafa ya Mikindani, akiwasilisha hoja zake kwa mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego (hayupo pichani) alipofanya kikao cha kazi na wakazi hao ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero zao.


kimaendeleo katika tarafa yao lakini madiwani wanamuangusha kutokana na kutohudhuria, hivyo kumuomba mkuu wa mkoa kuwaambia umuhimu wa kushiriki mikutano hiyo na kama wana tofauti za kisiasa basi waziondoe kwasababu hazina tija kwa sasa.
Katika hatua hatua nyingine, Mkumilwa, alikemea tabia za baadhi ya wakazi wa mji wa Mikindani ya kutopenda kuwa na vyoo na kuamua kujisaidia katika nyumba za watu wacheche walionavyo au katika fukwe za bahari, na kuwataka wenyeviti kukemea vikali na kuhakikisha wakazi wanakuwa na vyoo.

Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, akiongea na mmoja wa wakazi wa kata ya Jangwani tarafa ya Mikindani, baada ya kufanya ziara na kufanya kikao cha kazi kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi.



Mkuu wa mkoa, alimwagiza afisa tarafa ya Mikindani, Francis Mkuti, kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja kila nyumba inakuwa na choo, ambapo aliahidi kurudi baada ya muda huo kukamilika kwa ajili ya kukagua utekelezwaji wa agizo lake.

Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, akizungumza na wakazi wa kata ya Jangwani katika tarafa ya Mikindani alipofanya kikao cha kazi na kusikiliza kero za wananchi.



“Hakuna binadamu hasiyeenda chooni uonge au kweli?..sasa wewe mtu mzima choo huna unaenda wapi, kinachotakiwa hapa ni kubadilika ndugu zangu zamani mlikuwa wenyewe lakini sasahivi hiyo pwani yote inalindwa na ndani ya muda mfupi mtaona hekaheka zake..sasa ndugu yangu ukutwe pale umevua nguo wewe mwanamke mwenzangu ukutwe pale itakuwaje? Maana yeke pwani yote sisi tunaseti darubini tutakuwa tunaiona masaa 24..” alisema Dendego.

No comments: