Saturday, April 23, 2016

Mbuga Fc yapangiwa Morogoro, Mabingwa Mikoa..

Wachezaji wa Mbuga Fc wakishangilia bao katika mchezo wa fainali ya ligi ya mkoa dhidi ya Korosho Fc. (PICHA; JUMA MOHAMED)


Wachezaji wa Mbuga na Korosho. (PICHA; JUMA MOHAMED)


Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mtwara (MTWAREFA) Athuman kambi, akiongea baada ya mchezo wa fainali ya ligi ya mkoa kati ya Mabingwa Mbuga Fc na Korosho.(PICHA; JUMA MOHAMED)

 Mabingwa wa mkoa wa Mtwara katika ligi ya mkoa, timu ya Mbuga Fc ya Magomeni mjini hapa, imepangiwa kituo cha Morogoro katika michuano ya ligi ya mabngwa wa Mikoa inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi mwezi Mei mwaka huu.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetangaza Mei 14, 2016 kuwa tarehe ya kuanza kwa Ligi ya Mabingwa wa mikoa (RCL) itakayozishirkisha bingwa wa kila mkoa kutoka katika mikoa 27 nchini.
Ligi hiyo ya mabingwa wa mikoa itachezwa katika vituo vine nchini, ambapo mshindi wa kila kundi atapanda moja kwa moja ligi daraja la pili (SDL) na mshindi wa pili mwenye matokeo mazuri kutoka kundi A, B na C.

Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally akiwahutubia wachezaji wa timu za Mbuga Fc na Korosho za Mtwara baada ya mchezo wa fainali. (PICHA; JUMA MOHAMED)


Kundi A kituo cha (Njombe) kutakua na mabingwa wa mikoa ya Ruvuma, Iringa, Mbeya, Rukwa, Katavi, Dar es salaam 3, Morogoro, Kundi B kituo cha (Morogoro) kitakua na mabingwa wa mikoa ya Pwani, Mtwara, Lindi, Dar es salaam 1, Dar es salaam 2, Tanga, na Singida.

Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally akikabidhi kombe la ubingwa wa mkoa kwa nahodha wa timu ya Mbuga Fc ya Mtwara. (PICHA; JUMA MOHAMED)


Kundi C kituo cha (Singida) kitakua na mabingwa wa mikoa ya Dodoma, Arusha, Kilimanjaro, Tabora, Kagera, Manyara, na Njombe, huku kundi D kituo cha (Kagera) kikiwa mabingwa wa mikao ya Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara na Kigoma.

CHANZO: TFF

No comments: