Halmashauri ya Mtwara imeongoza katika kufaulisha wanafunzi wa darasa la saba ambao wanatarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2016, baada ya kuwa yakwanza Kimkoa na nafasi ya 16 kitaifa.
Halmashauri hiyo imepanda kwa asilimia 15.8 kutoka katika ufaulu wa mwaka jana ambapo ulikua ni sawa na asilimia 71 huku mwaka huu ikipaa mpaka asilimia 86.8.
Masasi wameshindwa kupiga hatua na kujikuta kuwa katika nafasi ileile ambapo mwaka 2014 walipata asilimia 53 huku mwaka 2015 wakipata asilimia 53.2.
Nanyumbu wao, mwaka 2014 walipata asilimia 58 ambapo mwaka huu wameambulia asilimia 55.1 na kujikuta wakiporomoka kwa asilimia 3.1.
No comments:
Post a Comment