David De Gea |
Juma Mohamed
HABARI njema
kwa mashabiki wa Manchester United ni kwamba, mlinda mlango namba moja wa klabu
hiyo raia wa Hispania, David De Gea, amesaini mkataba wa miaka minne wa
kuendelea kukipiga Old Tafford mpaka mwaka 2019 ambao una kipengele cha
kuongeza mwaka mmoja.
Taarifa zilizotolewa leo na mtandao wa klabu hiyo zinasema
kuwa, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, alijiunga na United mwaka 2011
ambapo amecheza kwa mafanikio michezo 174 na kunyakua ubingwa wa Uingereza
mwaka 2013 kabla ya kutwaa tuzo mbili za mchezaji bora wa mwaka wa klabu hiyo
(Sir Matt Busby).
“Ninafuraha kuanza ukurasa mpya wa kuendelea kuitumkia
United..nina ‘enjoy’ kucheza pamoja na wachezaji wenye viwango vikubwa tukiwa
mbele ya mashabiki wetu. Man Utd ndio klabu pekee na Old Trafford ndio maali
pekee kwangu kuendeleza kazi yangu..” alisema De Gea.
Na kuongeza “ninaamini utakuwa ni msimu mgumu lakini
nitapambana kwa ajili ya kuisaidia timu kwa kusaidiana na wenzangu kufikia
mafanikio..” aliongeza.
Kwa upande wake, kocha wa mashetani wekundu hao, Muholanzi,
Luis Van Gaal, alisema “ninafuraha kusema David amesaini mkataba mpya. Huyu ni
mmoja wa magolikipa bora duniani..nisema tu kwamba atakuwa sehemu ya timu yetu
ka miaka mingine mingi tu” alisema.
Na kuongeza “David alikuwa na mchango mkubwa katika timu yetu
msimu uliopita, na alikuwa mchezaji bora wa klabu kwa miaka miwili
mfululizo..ni mchezaji maarufu ambaye anahitaji kujifunza zaidi na kutokana na
kuwa na umri mdogo, ana nafasi kubwa ya kucheza michezo mingi zaidi..” aliongeza
LVG.
SOURCE: MAN UTD.COM
No comments:
Post a Comment