Na Juma Mohamed.
Wapinzani wa
Barcelona katika fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya (UEFA), klabu ya
Juventus ya Turin, nchini Italia, imepata pigo ikiwa ni sku mbili kabla ya
kipute hicho, baada ya mlinzi wao wa kutumainiwa Giorgio Chiellin kuumia misuli
ya mguu wake wa kushoto akiwa mazoezini hapo jana.
![]() |
| Giorgio Chiellini |
Taarifa ya
klabu hiyo imethibitisha kukosekana kwa mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 30
ambaye kama angefanikiwa kucheza mchezo huo, angekutana kwa mara ya kwanza na
Luis Suarez, raia wa Argentina ambaye alimng’ata Chiellin katika fainali za
kombe la Dunia nchini Brazil, mwezi June mwaka jana.
SOURCE: UEFA


No comments:
Post a Comment