Friday, March 29, 2013

Mandela aendelea vizuri na matibabu


Bw. Nelson Mandela

Bw. Nelson Mandela aliyekuwa rais wa Afrika Kusini anapokea vizuri matibabu kufuatia kusumbuliwa tena na maambukizi kwenye mapafu. Msemaji wa rais Bw Mac Maharaj amesema Mandela anaendelea kutibiwa na kufanyiwa upimaji hospitalini, na ikulu inavishukuru vyombo vya habari na umma kwa ushirikiano wao katika kuheshimu faragha ya Mandela na familia yake. Bw. Mandela alilazwa usiku wa Jumatano.
Tuendelee kumuombea waungwana.

No comments: