Friday, March 29, 2013

Mahakama ya Misri yamwachia kwa muda waziri wa zamani wa mafuta


Bw. Sameh Fahmi
Mahakama ya Misri imeamua kumwachia kwa muda waziri wa zamani wa mafuta wa nchi hiyo Bw Sameh Fahmi ambaye anakabiliwa na kesi ya kusafirisha gesi nchini Israel kwa bei ya chini ya soko. 

Uamuzi wa mahakama hiyo umekuja baada ya Bw Fahmi kufungua malalamiko kwa kutumikia muda wa zaidi ya miezi 18 akiwa chini ulinzi, ambapo kwa mujibu wa sheria muda huo ni mrefu sana kuwekwa kizuizini.

No comments: