Wednesday, October 24, 2012

PATRICK AMOTE, RASHIDI MATUMLA, YASIN ABDALAH OSTADH NA MABONDIA WOTE KUTOKA DAR ES SALAAM, WAPO NJIANI WAKIELEKEA MTWARA KWAAJILI YA PAMBANO LA JUMA PILI

Msafara wa watu wapatao 15, kutoka Dar Es salaam, ukiongozwa na Rais wa Oganaizesheni ya Ngumi za kulipwa nchini Yasin Abdallah 'Ostadh', unatarajia kufika Mkoani Mtwara leo jioni, tayari kwa pambano la Juma Pili.
Katika msafara huo wamo mabondia Rashid Matumla wa Tanzania akiwa na Kocha wake na Patrick Amote wa Kenya nae pia yupo na Kocha wake, pamoja na mabondia wengine wa Dar Es salaam ambao watacheza mapambano ya utangulizi na mabondia wa Klabu ya Masumbwi ya Black Mamba ya Mtwara.

No comments: