Saturday, September 8, 2012

YANGA YAUA 4-0 DAR, KAVUMBANGU AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO JANGWANI



Yanga SC
Na Mahmoud Zubeiry
YANGA ya Dar es Salaam imeifunga mabao 4-0 Moro United iliyoshuka Daraja msimu uliopita kutoka Ligi Kuu, katika mchezo wa kirafiki kujiandaa na Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, inayoanza Septemba 15, mwaka huu, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Kijitonyama, Dar es Salaam.
Kavumbangu, amefungua
akaunti ya mabao Yanga leo
Mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Didier Kavumbangu leo amefungua rasmi akaunti yake ya mabao Yanga, baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi huo, mabao mengine yakitiwa kimiani na beki Juma Abdul na kiungo Shamte Ally.
Kocha wa Yanga, Tom Saintfiet raia wa Ubelgiji alitaka mechi moja dhidi ya timu inayocheza kama wapinzani wao wa kwanza katika Ligi Kuu, Prisons na pia katika Uwanja mbaya kama ambao atachezea mechi ya kwanza ya ligi hiyo, Sokoine mjini Mbeya na ndiyo maana timu hiyo imecheza mechi hiyo leo kwenye Uwanja huo.
Saintfiet ameridhika na kiwango cha timu na sasa anasema timu iko tayari kwa Ligi Kuu, akianza na Prisons iliyorejea Ligi Kuu msimu huu kwenye Uwanja wa Sokoine, Septemba 15.
Hiyo inakuwa mechi ya 11, Saintfiet anashinda Yanga katika mechi 12 tangu ajiunge nayo miezi miwili iliyopita.

REKODI YA SAINTFIET YANGA
1. Yanga Vs JKT Ruvu 2-0
2. Yanga Vs Atletico (Burundi) 0-2
3. Yanga Vs Waw Salam (Sudan Kusini) 7-1
4. Yanga Vs APR (Rwanda) 2-0
5. Yanga Vs Mafunzo (Z’bar) 1-1 (5-3penalti)
6. Yanga Vs APR (Rwanda) 1-0
7. Yanga Vs Azam 2-0
8. Yanga Vs African Lyon 4-0
9. Yanga Vs Rayon (Rwanda) 2-0
10. Yanga Vs Polisi (Rwanda) 2-1
11. Yanga Vs Coastal Union 2-1
12. Yanga Vs Moro United 4-0
 
SOURCE:BIN ZUBEIRY

No comments: