OKWI
MSHAMBULIAJI
wa kimataifa wa Simba Mganda Emmanuel Okwi anatarajia kwasili nchini kesho
kutoka kwao Uganda.
Okwi
alikuwa huko kwa ajili ya kuitumikia timu ya Taifa ya huko ‘The Cranes’ ambayo
leo ilikuwa na mechi ya kuwania kufuzu fainali za Afrika dhidi ya
Zambia.
Ofisa
habari wa Simba Ezekiel Kamwaga amesema kwamba wamekubaliana kimaandishi na
nyota huyo kwamba atatua leo na kuungana na wenzake wanaojiandaa na ligi kuu
bara itakayoanza kutimua vumbi Septemba 15 mwaka
huu.
Alisema
Okwi pia anatarajiwa kuwepo kwenye kikosi cha Simba kitakachoshuka dimbani
keshokutwa kuikabili Azam Fc katika mchezo wa kuwania ngao ya Jamii itakayopigwa
katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.
Kamwaga
aliongeza kuwa, kikosi cha timu hiyo kipo katika hali nzuri kikiendelea na
maandalizi yake kwa kufanya mazoezi katika viwanja vya TCC Chang’ombe chini ya
kocha wake Mserbia Milovan Cirkovic.
Aidha, Kamwaga aliongeza
kwamba mshambuliaji wao mwingine wa kimataifa Mzambia Felix Sunzu ambaye
alikwenda kwao baada ya kufiwa na dada yake naye alitarajiwa kurejea nchini leo.
No comments:
Post a Comment