Wednesday, September 5, 2012

TAMASHA KUBWA LA MASUMBWI LA KIMATAIFA KWA MARA YA KWANZA NDANI YA MKOA WA MTWARA

  
Tamasha la mchezo wa ngumi la kimataifa lililopewa jina la East Africa Professional Boxing and Music Entertinments,linataraji kufanyika mkoani Mtwara mnamo oktoba 27 mwaka huu.
   Tamasha hilo litakalofanyika katika ukumbi maarufu wa burudani mkoani Mtwara MAKONDE BEACH CLUB,limeandaliwa na Safari Media Group kupitia Safari Radio,na litawakutanisha mabondia wawili mashuhuri kutoka nchini Kenya ambao watapambana na mabondia wawili maarufu wa hapa nchini.
   Mwenyekiti wa tamasha hilo Mahamud Sinani amesema kwamba, lengo la kufanyika kwa tamasha hilo ni kupanua wigo wa mchezo wa ngumi hapa nchini, pamoja na kutoa hamasa kwa mabondia wachanga ambao wanachipukia
   Mabondia hao kutoka nchini Kenya ni Adul Noor ambae atapanda ulingoni kuonyeshana kazi na Mbwana Matumla katika pambano la uzito wa( Kg 58),wakati Mkenya mwingine Patrick Omote yeye atazichapa na Rashidi Matumla 'Snake Man' katika pambano la (Kg 72).
  Tamasha hilo linalosimamiwa na Oganization ya ngumi za kulipwa nchini (TPBO),litakuwa na mapambano ya utngulizi ambapo mabondia kutoka katika klabu ya masumbwi ya Black Mambaz ya Mkoani Mtwara, watapambana na mabondia kutoka jijini Dar Es salaam,huku pambano moja litakuwa la kuwania ubingwa wa (TPBO).
  Pia kutakuwa na burudani ya mziki kutoka kwa msanii mwenye nyota ya kupendwa na mashabiki wengi wa mziki wa kizazi kipya Juma Nature,ambae atatumbuiza mwishoni baada ya kumalizika kwa mapambano ya ngumi.
  
  

No comments: