Sunday, September 9, 2012

FERGUSON KUMDONDOSHA RONALDO TENA OLD TRAFFORD

 

Cristiano Ronaldo na kocha Sir Alex Ferguson wa Manchester United wakipozi na tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia wa Mwaka iliyotwaliwa na Ronaldo kabla ya kuanza kwa mechi ya Ligi Kuu ya England baina ya Manchester United na Wigan Athletic kwenye Uwanja wa Old Trafford mjini Manchester, England Januari 14, 2009.

SIR Alex Ferguson atawaomba wamiliki wa klabu ya Manchester United wavunje benki ili kumrejesha Cristiano Ronaldo kutoka Real Madrid.

Gazeti la Sunday Mirror limesema Ferguson atawaomba Manchester United kulipa chochote kinachotakiwa ili kumrejesha Ronaldo Old Trafford.

Hivi sasa SAF anataka kujua kama ni kweli straika huyo wa Ureno amedhamiria kutaka kuondoka Real Madrid.

Miaka mitatu tu iliyopita Ronaldo alijiunga na Real katika ada ya uhamisho iliyoweka rekodi ya dunia ya paundi milioni 80 akitokea Man United.

Hivi sasa, kama ni kweli anataka kuondoka, ­Ferguson ataiomba familia ya Glazer – ambayo inamiliki klabu ya Man United – kufanya kila iwezalo ili kumsajili tena straika huyo mwenye umri wa miaka 27.

Chanzo kutoka ndani ya Man United kilisema: "Kocha aliweka wazi wakati Ronaldo alipojiunga na Real kwamba kama ataondoka Bernabeu arudi Old Trafford.

"Ni uhamisho ambao utathibitisha kwamba Man United bado inaweza kupambana na yeyote kwa majina makubwa katika soka.

"Lakini, kwa sasa, ni Ronaldo tu anayejua kama yuko 'siriasi' kuhusu kuondoka Madrid au anawazingua tu."

No comments: