DIAMOND AMSHUKURU WEMA 'LIVE' KUMFUNDA KIINGEREZA
Diamond na Wema enzi za penzi la shatashata, ambalo sasa limebaki historia |
Diamond ameyasema hayo leo mchana katika kipindi cha XXL cha Clouds Radio- baada ya kuulizwa siri ya kujiamini kwake kuzungumza vema Kiingereza bila kitete alipokuwa akihojiwa BBA.
"Namshukuru sana mama yangu mzazi aliyenisomesha, lakini pia namshukuru Wema Sepetu English Course, kwa kweli alinisaidia sana wakati nipo naye kunifundisha kuzungumza Kiingereza kwa kujiamini,"alisema Diamond.
Diamond anakuwa msanii wa pili kuzungumza hadharani kunufaika na lugha ya Kiingereza kutoka kwa Wema, baada ya marehemu Steven Kanumba naye kuwahi kusema hapo awali, alisaidiwa mno na Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006 kunyoosha lugha huyo.
UEFA YAMFUNGIA MECHI TATU JOHN TERRY
BEKI wa klabu ya Chelsea, John Terry, atazikosa mechi mbili msimu
ujao utakapoanza wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, kufuatia adhabu ya UEFA kumzuia
asicheze katika mechi tatu.
Tayari
aliikosa fainali dhidi ya Bayern Munich, baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu
katika mchezo wa nusu fainali, wakati Chelsea ilipopambana na Barcelona.
Lakini
UEFA sasa imeamua kumuongezea adhabu, kwa kumkataza kucheza katika mechi mbili
zaidi.
Terry
pia hatakuwepo katika mechi ya Kombe la Super dhidi ya washindi wa ligi ya
Europa, Atletico Madrid ya Uhispania, itakayochezwa mwezi Agosti, na vile vile
mechi ya kwanza ya Chelsea katika hatua ya makundi ya kufuzu kwa ligi ya klabu
bingwa Ulaya.
Terry
na Chelsea wana muda wa siku tatu kuamua ikiwa watakata rufaa au la kufuatia
uamuzi huo.
Terry,
mwenye umri wa miaka 31, alitolewa kadi nyekundu na mwamuzi, kufuatia
kushindilia goti lake dhidi ya mchezaji wa Barca, Alexis Sanchez, pasipo hata
mpira kuwa karibu, wakati Chelsea ilikuwa tayari imefungwa bao 1-0 usiku
huo.
Aliwaomba
msamaha wenzake kwa kuwaletea fedheha.
Hata
hivyo licha ya kuondolewa Terry katika mechi hiyo, hatua hiyo haikuinyima
Chelsea ushindi, kwani hatimaye iliondoka kwa sare ya 2-2, na katika uwanja wa
Nou Camp, waliibuka washindi kwa jumla ya magoli 3-2.
Kisha
baada ya hapo walipata ubingwa wao wa kwanza katika fainali ya klabu bingwa,
licha ya kuwakosa wachezaji mahiri Terry, Ramires, Branislav Ivanovic na Raul
Meireles.
MAGOMA AZIKWA MABOVU
BINGWA
wa zamani wa dunia wa ngumi za kulipwa uzito wa Super Fly, aliyekuwa
akitambuliwa na WBU, Magoma Shaaban Ngereza, aliyefariki dunia usiku wa jana
katika hospitali ya Bombo, mkoani Tanga, amezikwa jioni ya leo katika makaburi
ya Mabovu, Tanga.
Bondia
maarufu wa zamani nchini, Ally Bakari ‘Championi’ ameiambia BIN
ZUBEIRY mchana wa leo kwamba taarifa hizo amezipata kutoka kwa famili ya
marehemu.
Magoma
(pichani
kushoto)
aliyezaliwa Oktoba 21, mwaka 1980 mjini Tanga, amefariki majira ya saa 12
jioni.
Championi alisema kwamba
Magoma alikuwa anaumwa kwa muda mrefu na siku nne zilizopita alizidiwa na
kukimbizwa katika hospitali hiyo, kabla ya umauti kumfika leo.
Hadi
anafariki dunia, Magoma (pichani kushoto) alikuwa amepigana jumla ya mapambano
16, akishinda 13, manane kati ya hayo kwa Knockout (KO), amepigwa matatu na yote
kwa KO na hakuwahi kutoka sare.
Magoma
alipanda ulingoni kwa mara ya mwisho Julai 21, mwaka 2006 na Eugen Sorin Tanasie
mjini Timisoara, Romania katika pambano ambalo alipigwa kwa Technical Knocout
(TKO) raundi ya pili.
Taji
lake la kwanza kutwaa lilikuwa ni la IBF Afrika, Septemba 12, mwaka 1998
akimpiga Mkenya Joseph Waweru kwa KO raundi ya kwanza, Uwanja wa Mkwakwani,
Tanga.
Mei 11,
mwaka 2000 alimpiga bondia ‘matata sana’ Totin Lukunim wa Thailand na kutwaa
taji la IBF Intercontinental, uzito wa Super Fly kwenye ukumbi wa PTA, Temeke,
Dar es Salaam.
Agosti
3, mwaka 2001 ndipo alitwaa ubingwa wa dunia wa WBU baada ya kumpiga Ferid Ben
Jeddou wa Tunisia kwa TKO raundi ya sita mjini Avezzano, Abruzzo, Italia, kabla
ya kupoteza taji hilo kwa kupigwa na Gabula Vabaza Julai 26, mwaka 2002 katika
ukumbi wa Hemingways Casino, East London, Eastern Cape, Afrika Kusini kwa KO
raundi ya kwanza.
Mei 25,
mwaka 2003 alipigwa na Mtanzania mwenzake, Mbwana Matumla kwenye ukumbi wa
Diamond Jubilee, Dar es Salaam kwa TKO raundi ya nne.
Alijiunga rasmi na ngumi za
kulipwa mwaka 1996, pambano lake la kwanza akicheza Juni 3, mwaka huo na kumpiga
Athumani Omari kwa pointi, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Mungi
aiweke pema peponi roho ya marehemu. Amin
BREAKING NEWS: SIMBA KUMTEMA MACHAKU
KIUNGO mshambuliaji wa Simba,
Salum Machaku (pichani kulia) anaweza kutolewa kwa mkopo kwa nusu msimu,
ili ajifundishe adabu- kwani hivi sasa mabega yamepanda mno juu.
Habari ambazo BIN
ZUBEIRY imezipata kutoka ndani ya Simba, zimesema kwamba Machaku amekuwa
akijisikia mno baada ya kufanya vizuri kidogo msimu huu akiwa na jezi ya Wekundu
wa Msimbazi, kiasi kwamba amekuwa akidharau hadi viongozi.
Kiongozi mmoja wa juu wa
Simba, aliiambia BIN ZUBEIRY wiki hii kwamba uongozi ulifanya
jitihada kubwa za kumbadili kitabia Machaku, ikiwemo kumuweka chini ya mchezaji
anayeogopwa na wachezaji wote, Haruna Moshi ‘Boban’, lakini
ikashindikana.
“Sasa tunataka tumpe nafasi ya
mwisho, tumpeleke kwa mkopo klabu nyingine akacheze mzunguko mmoja tu,
akijirekebisha, tunamrudisha, ikishindikana ndio imetoka,”alisema kiongozi
huyo.
Wakati huo huo, Machaku ni
kati ya wachezaji ambao wamo kwenye orodha ya nyota wanaotakiwa na mahasimu wa
jadi wa Simba, Yanga. Na katika siku za karibuni, Machaku amekuwa karibu mno na
kipa wa Yanga, Shaaban Hassan Kado ambaye waliwahi kucheza naye pamoja Mtibwa
Sugar na timu ya taifa.
Thursday, May 31, 2012
MAN UNITED WAWANIA BEKI AMBAYE BARCA WANAMTAKA
Tetesi za Ijumaa magazeti Ulaya
MANCHESTER UTD WATAKA KUSAJILI BEKI WA BARCELONA
KOCHA Brendan Rodgers,
ambaye anatarajiwa kutambulishwa rasmi leo kuwa kocha wa Liverpool, anaweza
kuondoka na wachezaji wake watatu wa zamani: Scott Sinclair, mwenye umri wa
miaka 23, Gylfi Sigurdsson, miaka 22, na Ashley Williams, miaka
27.
KIUNGO
wa Swansea, Joe Allen, mwenye umri wa miaka 22, pia ameorodheshwa katika orodha
ya wachezaji wanaokwenda Anfield - ingawa kinda huyo bado mkataba wa miaka
mitatu na katika klabu yake hiyo ya Wales na anaweza kuigharimu Liverpool pauni
Milioni 10.
KLABU
ya Manchester United imejiunga katika mbio za kuinasa saini ya kiungo wa
Valencia, Jordi Alba, mwenye umri wa miaka 23. Beki huyo wa kushoto pia
anawaniwa na Barcelona.
KLABU
ya Bayer Leverkusen imeghairi mpango wa kumchukua Dimitar
Berbatov, mwenye umri wa miaka 31, labda klabu yake ya sasa, Manchester United
imtoe bure mshambuliaji wake huyo.
KLABU
ya Manchester City inajiandaa kuwapiga bao wapinzani wao wa Jiji, Man United
katika kumsajili kiungo Mholanzi, Wesley Sneijder, mwenye umri wa miaka 27,
kutoka Inter Milan.
MSHAMBULIAJI
wa Norwich, Grant Holt, mwenye umri wa miaka 31, anajiandaa kumfuata kocha wake,
Paul Lambert katika klabu ya Aston Villa aliyohamia.
MOURINHO AMFAGILIA RODGERS
KOCHA
wa Real Madrid, Jose Mourinho amemwagia ujiko kocha mwenzake wa zamani Chelsea,
Brendan Rodgers kwamba atarejesha enzi za furaha katika klabu ya
Liverpool.
MWENYEKITI
wa Wigan, Dave Whelan anaamini Aston Villa si klabu tosha kwa Roberto
Martinez.
KOCHA
wa klabu ya Tottenham, Harry Redknapp atataka kujua kama bado anaungwa mkono na
bodi ya klabu hiyo, kabla ya kuamua kufuata ofa ya kwenda kufundisha soka Qatar
anakotakiwa kwa maslahi mazuri.
KOCHA
wa zamani wa Chelsea, Andre Villas-Boas alilipwa fidia ya pauni ya Milioni 12
alipofukuzwa katika klabu hiyo, Machi mwaka huu.
KLABU
ya Norwich iko tayari kumchukua kocha wa Celtic, Neil Lennon akazibe pengo la
Paul Lambert, anayejiandaa kutua Aston Villa.
CHELSEA WAJIANDAA NA ZIARA YA MAREKANI
NYOTA
wa klabu ya Chelsea, wameanza kujiandaa kwa ziara ya kujiandaa na msimu mpya
nchini Marekani.
STARS WATUA ABIDJAN, KIM POULSEN ASEMA MAMBO MAGUMU
Wachezaji wa Stars wakati wakiondoka Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam kwenda Abidjan Alfajiri ya jana |
Na Boniphjace Wambura,
Abidjan
KIKOSI cha timu ya soka ya
taifa ya Tanzania, Taifa Stars kimewasili hapa Abidjan jana mchana huku Kocha
Mkuu wa timu hiyo Kim Poulsen akisema mechi dhidi ya Ivory Coast itakuwa
ngumu.
Stars yenye
wachezaji 21 ilikuwa iwasili hapa asubuhi, lakini ndege iliyobadilisha Nairobi
ilichelewa kuondoka kwa saa tatu. Mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya
Taifa Stars na wenyeji Ivory Coast (Tembo) itachezwa Juni 2 mwaka huu Uwanja wa
Felix Houphouet-Boigny kuanzia saa 11 kamili jioni ambapo Tanzania itakuwa saa 2
kamili usiku.
Licha ya
kwanza, Stars ililazimika kuacha wachezaji wawili dakika za mwisho (Haruna Moshi
na Nassoro Cholo), Kim amesema kikosi chake ambacho kimefikia hoteli ya Ibis
bado kimejipanga vizuri kwa ajili ya mechi hiyo.
“Tunaiheshimu
Ivory Coast kwa vile ni timu ambayo inaundwa na baadhi ya wachezaji nyota wa
dunia kama akina Drogba (Didier) na Yaya (Toure), lakini wajiandaa kupata wakati
mgumu kutoka kwetu,” amesema Kim ambayo kikosi chake baada ya kuwasili hapa
kilipata fursa ya kufanya mazoezi jioni.
Kikosi cha
Stars kinaongozwa na Nahodha wake Juma Kaseja akisaidiwa na Aggrey Morris.
Wachezaji wengine waliopo hapa na kikosi hicho ni Mwadini Ally, Deogratius
Munishi, Amir Maftah, Erasto Nyoni, Kelvin Yondani, Waziri Salum, Shomari
Kapombe na Juma Nyoso.
Jonas
Mkude, Mwinyi Kazimoto, Salum Abubakar, Shabani Nditi, Edward Christopher,
Mrisho Ngasa, Frank Domayo, Mbwana Samata, Ramadhan Singano, Simon Msuva na John
Bocco.
Mbali ya
Kim, Benchi la Ufundi lina Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali
(Kocha wa makipa), Leopold Mukebezi (Meneja wa timu), Juma Mwankemwa (Daktari wa
timu), Frank Mhonda (Physiotherapist) na Alfred Chimela (Mtunza
vifaa).
Msafara wa
Stars hapa unaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) Crescentius Magori lakini pia yupo
Mwenyekiti wa Baraza la
Michezo la Taifa (BMT), Dioniz Malinzi ambaye amekuja kushuhudia mechi
hiyo.
BREAKING NEWS: BONDIA MAGOMA SHAABAN AFARIKI DUNIA
BINGWA wa zamani wa dunia wa
ngumi za kulipwa uzito wa Super Fly, aliyekuwa akitambuliwa na WBU, Magoma
Shaaban Ngereza amefariki dunia usiku huu katika hospitali ya Bombo, mkoani
Tanga, imeelezwa.
Bondia maarufu wa zamani
nchini, Ally Bakari ‘Championi’ ameiambia BIN ZUBEIRY usiku huu
kwamba, Magoma aliyezaliwa Oktoba 21, mwaka 1980 mjini Tanga, amefariki majira
ya saa 12 jioni.
Championi alisema kwamba
Magoma alikuwa anaumwa kwa muda mrefu na siku nne zilizopita alizidiwa na
kukimbizwa katika hospitali hiyo, kabla ya umauti kumfika leo.
Hadi anafariki dunia, Magoma
(pichani kushoto) alikuwa amepigana jumla ya mapambano 16, akishinda 13, manane
kati ya hayo kwa Knockout (KO), amepigwa matatu na yote kwa KO na hakuwahi
kutoka sare.
Magoma alipanda ulingoni kwa
mara ya mwisho Julai 21, mwaka 2006 na Eugen Sorin Tanasie mjini Timisoara,
Romania katika pambano ambalo alipigwa kwa Technical Knocout (TKO) raundi ya
pili.
Taji lake la kwanza kutwaa
lilikuwa ni la IBF Afrika, Septemba 12, mwaka 1998 akimpiga Mkenya Joseph Waweru
kwa KO raundi ya kwanza, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Mei
11, mwaka 2000 alimpiga bondia ‘matata sana’ Totin Lukunim wa Thailand na kutwaa
taji la IBF Intercontinental, uzito wa Super Fly kwenye ukumbi wa PTA, Temeke,
Dar es Salaam.
Agosti 3, mwaka 2001 ndipo
alitwaa ubingwa wa dunia wa WBU baada ya kumpiga Ferid Ben Jeddou wa Tunisia kwa
TKO raundi ya sita mjini Avezzano, Abruzzo, Italia, kabla ya kupoteza taji hilo
kwa kupigwa na Gabula Vabaza Julai 26, mwaka 2002 katika ukumbi wa Hemingways
Casino, East London, Eastern Cape, Afrika Kusini kwa KO raundi ya
kwanza.
Mei
25, mwaka 2003 alipigwa na Mtanzania mwenzake, Mbwana Matumla kwenye ukumbi wa
Diamond Jubilee, Dar es Salaam kwa TKO raundi ya nne.
Alijiunga rasmi na ngumi za
kulipwa mwaka 1996, pambano lake la kwanza akicheza Juni 3, mwaka huo na kumpiga
Athumani Omari kwa pointi, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Mungi aiweke pema peponi roho
ya marehemu. Amin.
VIFAA VINAVYOMULIKWA EURO 2012, VYAWEZA KUHAMA BAADA YA MASHINDANO
PSG iko tayari kumng'oa Rooney Man United kwa Euro Milioni 150 |
Man City iko tayari kumng'aoa Van Persie Arsenal kwa dau la pauni milioni 50 |
JORDI ALBA | Valencia & Hispania, Beki, Miaka 23 |
Read more on Alba |
|
ANDREY ARSHAVIN | Arsenal & Urusi, Mshambuliaji, Miaka 31 |
Read more on Arshavin |
|
THEO GEBRE SELASSIE | Slovan Liberec & Jamhuri
ya Czech, Beki, Miaka
25 |
Read more on Gebre Selassie |
|
SEBASTIAN GIOVINCO | Parma & Italia,
Mshambuliaji, Miaka
25 |
Read more on Giovinco |
|
BENEDIKT HOWEDES | Schalke & Ujerumani, Beki, Miaka 24 |
Read more on Howedes |
|
ROBERT LEWANDOWSKI | Dortmund & Poland,
Mshambuliaji, Miaka
23 |
Read more on Lewandowski |
|
JAVI MARTINEZ | Athletic Bilbao & Hispania,
kiungo, Miaka 23 |
Read more on Martinez |
|
YANN M'VILA | Rennes & Ufaransa, kiungo, Miaka
21 |
Read more on M'Vila |
|
ROLANDO | Porto & Ureno, beki, miaka
26 |
Read more on Rolando |
|
KEVIN STROOTMAN | PSV & Uholanzi, kiungo, miaka 22 |
Read more on Strootman |
|
OLA
TOIVONEN | PSV & Sweden, kiungo, miaka
25 |
Read more on Toivonen |
|
GREGORY VAN DER WIEL | Ajax & Uholanzi, beki,
miaka 24 |
Read more on Van der Wiel |
|
ANDRIY VORONIN | Dinamo Moscow & Ukraine,
mshambuliaji, miaka
32 |
Read more on Voronin |
|
No comments:
Post a Comment