Monday, May 28, 2012

KOCHA JUVENTUS AKAMATWA NA POLISI KWA KUPANGA MATOKEO, KAMBI YA ITALIA EURO 2012 YAVAMIWA


28 May 2012Last updated at 10:02 GMT
NAHODHA wa Lazio amekamatwa na polisi kwa uchunguzi wa kupanga matokeo mchezoni.
Kiungo Stefano Mauri, mwenye umri wa miaka 32, alishikiliwa kwa pamoja na kiungo wa zamani wa Genoa, Omar Milanetto, polisi ilisema.
Kocha wa Juventus, Antonio Conte, ambaye ameiongoza klabu hiyo kutwaa ubingwa wa Serie A katika msimu wake wa kwanza kazini, ni miongoni mwa waliohojiwa na polisi.
Maofisa wa Polisi walitembelea pia kambi ya mazoezi ya timu ya taifa ya Euro 2012 kumuhoji beki Domenico Criscito, mwenye umri wa miaka 25.
Polisi walipekua nyumba zaidi ya 30, zikiwemo za wachezaji, makocha na viongozi wa klabu za Serie A, Serie B na madaraja ya chini zaidi.
Polisi ilisema Conte alifanyiwa uchunguzi juu ya shaka ya kushiriki mchezo mchafu wa kupanga matokeo mchezoni kati ya klabu yake ya awali, Siena na Novara, Aprili mwaka 2011. Watu wengine watano walikamatwa pia nchini Hungary kwa kuhisiwa kuwa sehemu ya mchezo huo mchafu, unaopigwa vita kali.

MILIONEA WA YANGA ANENA BUSARA TUPU


Bin Kleb akimkabidhi jezi Haruna Niyonzima baada ya kumsajili mwaka jana mjini Kigali 'kwa bei chafu' kutoka APR ya Rwanda

MDAU wa soka nchini, Abdallah Ahmed Bin Kleb ameomba ijitokeze kampuni ya kuwadhamini marefa wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara, ili kuwawezesha kujimudu na kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY usiku huu, Bin Kleb aliyekuwa Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, kabla ya kujiuzulu alisema kwamba marefa wa Tanzania wanafanya kazi katika mazingira magumu na wanalipwa posho kidogo mno na TFF.
“Nasikia wanalipwa Sh. 70,000, hizi ni fedha kidogo sana, haziwezi kuwatosheleza kujikimu, naomba ijitokeza kampuni maalum, kwa ajili ya kuwadhamini marefa wa Ligi Kuu, kwa sababu kwa kufanya hivyo kampuni zitanufaika kwa sababu watatangazwa kibiashara,”alisema.
Bin Kleb alisema kwamba, wakati mwingine watu wanakosea kuwatupia shutuma nyingi waamuzi kwamba wanapenda rushwa, ingawa hutokea hatakwa waamuzi walio waadilifu wakaingia kwenye mitego kwa sababu ya hali halisi inayowakabili.
Aidha, Bin Kleb alisema anastaajabishwa mno na vyombo vya habari nchini, kuelekeza nguvu zao katika mechi za Ligi Kuu zinazochezwa Dar es Salaam pekee, wakati mikoani ndiko kuna mambo mengi ‘ya ajabu’.
“Unakuta Televisheni zinaonyesha mechi za Dar es Salaam pekee, wakati huko mikoani ndiko kuna mambo ya ajabu kweli kweli, ambayo yanatakiwa yaripotiwe ili yakomeshwe, kwa hivyo natoa haya mawili kama changamoto kwa maslahi ya soka yetu,”alisema Bin Kleb.

CECH ASAINI MKATABA MPYA CHELSEA MIAKA MINNE



EPL:Petr Cech, Chelsea v Newcastle United
Cech



KIPA wa Chelsea, Petr Cech amemwaga wino akitia saini mkataba mpya wa kuendelea kuichezea klabu hiyo bingwa Ulaya kwa miaka minne zaidi.
Kipa huyo wa kimataifa wa Czech, alijiunga na The Blues mwaka 2004, akitokea Rennes Ufaransa kwa dau la pauni Milioni 9 na hadi sasa amedaka mechi 369 katika klabu hiyo, akiiwezesha kutwaa mataji matatu ya Ligi Kuu ya England, manne ya FA, mawili ya Carling na moja la Ligi ya Mabingwa na s
asa atakuwa Stamford Bridge hadi mwaka 2016.


"Ninafurahi mno kuwa ni sehemu ya klabu hii maarufu kwa kipindi cha miaka mine zaidi," alielezea mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30.
"Ninatumaini miaka hiyo minne ijayo itakuwa ni sawa na miaka minane ambayo nimekuwa nikikichezea klabu."
Cech, ambaye mkataba wake wa awali ulikuwa umalizike mwaka ujao, ni mchezaji muhimu kwa Chelsea
Cech pia alitangazwa kama mchezaji bora zaidi wa Chelsea mwaka jana, 2010/11.
"Chelsea inatambua kikamilifu mchango muhimu kutoka kwa Petr wakati huu wa klabu kupata ufanisi wake mkubwa zaidi katika historia yake," alielezea mkurugenzi mkuu wa Chelsea, Ron Gourlay.
Kipa msaidizi wa Cech, Thibaut Courtois kutoka Ubelgiji, huenda akaachiwa mechi zaidi za ligi kuu ya Premier ili kujinoa zaidi, baada ya kuonyesha uhodari wake akiwa mchezaji wa mkopo katika klabu ya Uhispania ya Atletico Madrid, ijapokuwa kijana huyo wa miaka 20 huenda akaazimwa kwa timu nyingine kwa muda mfupi.
Courtois alijiunga na Chelsea kutoka klabu ya Racing Genk, mwezi Julai mwaka jana, na kwa kuelekea Uhispania na kutofungwa, aliiwezesha klabu ya Atletico Madrid kuibuka mabingwa wa klabu ya Europa mapema mwezi huu.

VIWANJA VYA EURO 2012 NA WASIFU WAKE


Euro 2012 venues map
27 March 2012Last updated at 12:44 GMT

Euro 2012: Viwanja na maelekezo Fainali za Mataifa ya Ulaya...

FAINALI za Kombe la Mataifa UlayaThe 2012 zitachezwa katika viwanja nane, vinne nchini Poland na vinne Ukraine.
Viwanja vitano vipya vimetengenezwa maalum kwa ajili ya michuano hiyo - na vingine vitatu vimefanyiwa ukarabati wa uhakika.
Fainali hizo zinaanza Juni 8 kwa wenyeji washiriki Poland kufungua dimba na Ugiriki katika Uwanja wa Taifa wa Warsaw, na kufikia tamati Julai 1katika Uwanja wa Olimpiki mjini Kiev, Ukraine.
Hapa BIN ZUBEIRY kwa msaada wa BBC Sport inakuletea viwanja ambavyo vitatumika kwa fainali hizo na wasifu wake.

Warsaw

National Stadium, Warsaw
KUJENGWA: 2011, WANAOUTUMIA: Timu ya taifa Polande accessible player and disable flyout menus
BBC News looks inside Warsaw's new national stadium
MECHI ZITAKAZOCHEZWA HAPA: Mechi tatu za Kundi A, ya ufunguzi kati ya Poland Ugiriki Juni 8, Poland na Urusi Juni 12, na Ugiriki na Urusi Juni 16.
UMBALI: Kutoka Kiev: Kilomita 820.

Wroclaw

Municipal Stadium (Stadion Miejski), Wroclaw
KUJENGWA: 2011
WANAOUTUMIA: Slask Wroclaw
MECHI ZITAKAZOCHEZWA HAPA: Kundi A
UMBALI: Kutoka Warsaw: kilomita 350 na kutoka Kiev kilomita 1,090.

Gdansk

PGE Arena, Gdansk
KUJENGWA: 2011
WANAOUTUMIA: Lechia Gdansk
MECHI ZITAKAZOCHEZWA HAPA: Kundi C.
DUMBALI: Kutoka Warsaw: Kilomota 345 na kutoka Kiev kilomita 1,190.

Poznan

City Stadium (Stadion Miejski), Poznan
KUJENGWA: 1980 (Kukarabatiwa 2010)
WANAOUTUMIA: Lech Poznan na Warta Poznan
MECHI ZITAKAZOCHEZWA HAPA: Kundi C
UMBALI: Kutoka Warsaw: Kilomita 320 na kutoka Kiev kilomita 1,140.

Kiev

Olympic Stadium (Olimpiysky Stadium), Kiev
KUJENGWA: 1923 (Kukarabatiwa 2011)
WANAOUTUMIA: Timu ya taifa ya Ukraibe.
MECHI ZITAKAZOCHEZWA HAPA: Kundi D
UMBALI: Kutoka Warsaw: kilomita 820.

Donetsk

Donbass Arena, Donetsk
KUJENGWA: 2009
WANAOUTUMIA: Shakhtar Donetsk
MECHI ZITAKAZOCHEZWA HAPA: Kundi D
UMBALI kutoka Kiev: Kilomita 700 na kutoka Warsaw kilomita 1,465.

Kharkiv

Metalist Stadium (Oblast Sports Complex Metalist), Kharkov
KUJENGWA: 1926 (Kukarabatiwa 2009)
WANAOUTUMIA: FC Metalist Kharkiv
MECHI ZITAKAZOCHEZWA HAPA: Kundi B.
UMBALI: Kutoka Kiev kilomita 480 na kutoka Warsaw kilomita 1,250.

Lviv

Arena Lviv, Lviv
KUJENGWA: 2011
WANAOUTUMIA: FC Karpaty Lviv
MECHI ZITAKAZOCHEZWA HAPA: Kundi B
UMBALI: Kutoka Kiev kilomita 540 na kutoka Warsaw kilomita 385.

GARETH BARRY AENGULIWA ENGLAND KIKOSI CHA EURO


England's Gareth Barry

KIUNGO Gareth Barry ameondolewa kwenye kikosi cha timu ya taifa kwa ajili ya Euro 2012, kwa sababu ya majeruhi ya nyonga, Chama cha Soka kimethibitisha.
Kiungo huyo England mwenye umri wa miaka 31, alifanyiwa vipimo mapema leo, ambavyo vimethibitisha ana maumivu makubwa.
"Ninasikitishwa sana kumpoteza Gareth," alisema kocha Roy Hodgson. "Nina uhakika ataendelea kuwa sehemu ya kikosi cha England baada ya Euros."
Hodgson amemuita beki wa Everton, Phil Jagielka kuchukua nafasi ya Barry.
"Kikosi cha mwisho cha England cha wachezaji watatu lazima iwe kimewasilishwa kwa ajili ya fainali hizo za Poland na Ukraine mchana wa kesho.
Barry, ambaye ameichezea tmu ya taifa mechi 50, alilazimika kutoka nje baada ya dakika 30 tu baada ya kuingia akitokea benchi katika mechi ya kirafiki na Norway mjini Oslo, Jumamosi.
Uamuzi wa Hodgson kumuita Jagielka unaweza kumfanya Phil Jones ahamie kwenye nafasi ya kiungo, ambako aliwahi kucheza wakati katika klabu yake, Manchester United mwishoni mwa msimu.
Bado wachezaji Danny Welbeck na Glen Johnson, ambao wamepona hivi karibuni maumivu ya kifundo cha mguu wanaangaliwa afya zao, na wawili hao wanatarajiwa kuwasili kambini, Watford kesho.
Scott Parker pia alikuwa majeruhi, lakini amethibitisha yuko fiti akitokea benchi dakika ya 55 katika mechi ya ushindi wa England wa 1-0 dhidi ya Norway mwishoni mwa wiki.


MISS DAR INTER COLLEGE MAZOEZINI

SHINDANO la Miss Dar Inter College 2012 linatarajiwa kufanyika Juni 8, mwaka huu katika ukumbi wa San Sirro, Sinza, Dar es Salaam likisindikizwa na burudani baab kubwa, kutoka kwa wasanii na vikundi ambavyo vitatajwa baadaye, kwa mujibu wa Dina Ismail, Mratibu wa shindano hilo.
Vimwana 15 wanaendelea na mazoezi, chini ya mwalimu wao, Marylidya Boniphace, Miss Dar Inter College 2009 kwenye hoteli ya Lamada, Ilala mjini Dar es Salaam.
BIN ZUBEIRY ilitembelea kambi ya warembo hao jioni ya leo, na kukuta totoz zisizopungua nane zikijinoa, wakati warembo wengine walikuwa wana udhuru. Hebu cheki totoz na jiulize kwa njini Juni 8 usiende San Sirro kucheki swaga zao.




TEVEZ ATAKIWA KWA UDI NA UDUMBA AC MILAN



Gossip logo
28 May 2012Last updated at 06:54 GMT

Monday's gossip column

IVANOVIC AITAMANI OFA YA REAL MADRID, LAKINI...

BEKI wa Chelsea, Branislav Ivanovic, mwenye umri wa miaka 28, anavutiwa na ofa ya mabingwa wa Hispania, Real Madrid ingawa amesema anafurahi kubaki Stamford Bridge.
WAKALA wa mchezaji anayetakiwa na klabu ya Manchester City, Thiago Silva, mwenye umri wa miaka 27, amesema beki huyo anaweza kukubali kuondoka San Siro ikiwa AC Milan itataka kumuuza.
KLABU ya AC Milan inataka kumsajili mshambujliaji wa Manchester City, Carlos Tevez, mwenye umri wa miaka 28, baada ya kukwama kumsajili Muargentina huyo Januari.
Manchester United defender Michael Keane
Michael Keane has represented Republic of Ireland at youth levels
KOCHA aliyekalia kuti kavu Blackburn, Steve Kean anataka kumsajili kinda wa Manchester United, mwenye umri wa miaka 19, pacha Michael Keane kwea mkopo wakati Rovers ikijiandaa na Ligi Daraja la Kwanza.
MSHAMBULIAJI wa Manchester City, Sergio Aguero, mwenye umri wa miaka 23, kwa dau la pauni Milioni 50 anawaniwa na klabu ya Real Madrid, lakini amegoma kuhama Etihad. "Maisha yangu yapo Manchester City. Nataka kubaki hapa," alisema.
MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Nicklas Bendtner, mwenye umri wa miaka 24, amethibitisha yupo kwenye mazungumzo na klabu kadhaa juu ya mpango wa kuhama Emirates.

HODGDON KWENDA BRAZIL

KOCHA wa England, Roy Hodgson amejipanga sawa sawa kwa ajili ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya, Euro 2012 ili afanye vizuri na kujitengenezea mazingira ya kuwa kocha wa muda mrefu wa timu hiyo.
KOCHA wa England, Roy Hodgson atasafiri kwenda Brazil moja kwa moja baada ya mashindano ya Euro 2012, kwenda kukagua sehemu ambayo itafaa kwa Three Lions kuweka kambi ya kujiandaa na Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini humo.
BEKI wa Fulham, raia wa Norway, Brede Hangeland, mwenye umri wa miaka 30, amesema wachezaji wa England wanatakiwa kudhihirisha ubora wao kwenye Euro 2012, baada ya msimu mrefu wa mafanikio.
NYOTA Scott Parker, mwenye umri wa miaka 31, amezungumzia anavyojisikia vizuri baada ya kuwa fiti kwa ajili ya kuiwakilisha England kwenye Euro 2012, baada ya kuumizwa na klabu yake kukosa tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao.
Tottenham player Giovani Dos Santos
Giovani Dos Santos.
KIUNGO Frank Lampard, mwenye umri wa miaka 33, anakabiliwa na mkanganyiko wa mawazo kwenye Euro 2012 baada ya kocha wa England, Roy Hodgson kuamua chaguo lake la kwanza katika safu ya kiungo ya timu ni Steven Gerrard na Scott Parker.
BEKI wa zamani wa Arsenal na Tottenham, Sol Campbell amewaonya mashabiki wa England kutokwenda kwenye fainali za Euro 2012, kwa sababu wanaweza kurejea na maumivu.
NYOTA wa Tottenham, mwanaoska wa kimataifa wa Mexico, Giovani Dos Santos, mwenye umri wa miaka 23, anaweza akaomba kuondoka, vinginevyo ahakikishiwe kuchezeshwa kwenye Uwanja wa White Hart Lane.
KLABU ya Liverpool itafanya mazungumzo na kocha wa Swansea, Brendan Rodgers katika kukamilisha msako wao wa kumtafuta mrithi wa Kenny Dalglish.
MMILIKI wa Wigan, Dave Whelan yuko tayari kutimiza masharti ya kocha Roberto Martinez, ili kumzuia asihamie Liverpool au Aston Villa.
THE Latics wanatarajiwa kufanya mazungumzo na Waandishi wa Habari, ili Martinez aseme kama atapenda kubaki au kuondoka.

MUGABE CHELSEA DAMU

RAIS wa Zimbabwe, Robert Mugabe amesema yeye ni shabiki wa Chelsea tangu klabu hiyo ya London, itwae taji la Ligi ya Mabingw3a Ulaya kwa kuifunga Bayern Munich.

SERENGETI YAZIDI KUWANUFAISHA WATANZANIA

Ni meneja wa masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti kanda ya ziwa bw Patrick kisaka akikabidhi za bajaj kwa mshindi wa bajaj katika promosheni ya VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO na SBL, Bw Godfrey Shao mkazi wa mkoa wa mwanza ambaye alijishindia pikipiki ya matairi matatu( BAJAJ) kupitia bia ya Tusker Lager

Mshindi wa Bajaj bw Godfery Shao ndani ya bajaj akipongezwa na wafanyakazi, wawakilishi, wapenzi na wadau wa kampuni ya bia ya Serengeti baada ya kukabidhiwa bajaj mpya kabisa


Sunday, May 27, 2012

DROGBA AONGOZA ORODHA YA WAAFRIKA BORA 20 KUWAHI KUCHEZA ENGLAND

Didier Drgoba, ambaye SuperSport.com imempa namba moja katika orodha ya wanasoka bora 20 wa Afrika waliowahi kucheza Ligi Kuu ya England, ikitimiza miaka 20 mwaka huu. Tazama orodha kamili chini.


1. Didier Drogba - Ivory Coast (Chelsea)
2. Nwankwo Kanu - Arsenal (West Brom, Portsmouth)
3. Michael Essien - Ghana (Chelsea)
4. John Obi Mikel - Nigeria (Chelsea)
5. Tony Yeboah - Ghana (Leeds)
6. Lucas Radebe - South Africa (Leeds)
7. Emmanuel Eboue - Ivory Coast(Arsenal)
8. Austin Jay-Jay Okocha - Nigeria (Bolton)
9. Lauren Etama-Mayer - Cameroon (Arsenal)
10. Stephen Pienaar - South Africa (Everton, Tottenham Hotspur)
11. Kolo Toure - Ivory Coast (Arsenal, Manchester City)
12. Yaya Toure - Ivory Coast (Manchester City)
13. Alex Song - Cameroon (Arsenal)
14. Peter Ndlovu - Zimbabwe (Coventry)
15. Papiss Demba Cisse - (Newcastle)
16. Yakubu Aiyegbeni – Nigeria (Portsmouth, Middlesbrough, Everton, Blackburn Rovers)
17. Emmanuel Adebayor - Togo (Arsenal, Manchester City, Tottenham)
18. Joseph Yobo - Nigeria (Everton)
19. Bruce Grogbelaar - Zimbabwe (Liverpool, Southampton)
20. Peter Osaze Odemwingie - Nigeria (West Brom)

POULSEN MDOGO AOMBA APEWE MUDA STARS

Kim Poulsen

KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Kim Poulsen amesema timu yake inaweza kufanya vizuri, lakini lazima wapewe muda.
Gazeti la Habari Leo, limeandika leo kwamba kutokana na hali hiyo amewaomba mashabiki nchini kuwa wavumilivu na kwamba ipo siku wataikubali na kuanza kuwashangilia wachezaji.
“Ni mwanzo mzuri wa safari yangu, kutoka sare nadhani ni mwanzo mzuri, sio matokeo mabaya kwangu na wala sio matokeo mabaya kwa Malawi, nahitaji kupewa muda zaidi,”alisem Kim baada ya mchezo wa kirafiki kati ya Stars na Malawi juzi uliomalizika kwa timu hizo kutofungana.
Alisema amefurahishwa na kiwango ambacho timu yake ilikionesha na kuomba kupewa
muda zaidi ili ifanye vizuri kwani kikosi chake bado ni kichanga na kinaundwa na wachezaji wengi chipukizi hivyo hawezi kuibadilisha timu hiyo kipindi cha wiki moja tokea aanze kuifundisha timu hiyo.
Kocha huyo aliyekuwa akifundisha timu za taifa za vijana aliwataka wachezaji wa timu hiyo
kucheza vizuri muda wote ili kuwanyamazisha mashabiki wachache waliokuwa wakiizomea
kwenye mchezo huo.
“Ukiona mashabiki wanazomea ujue bado haujawafurahisha, nafikiri wakicheza vizuri hawatazomewa, naelewa hisia za mashabiki kuwa wanataka timu ishinde na ichezea vizuri lakini hilo lisipotokea ni wazi watazomea,”alisema Kim.
Taifa Stars itacheza na timu ya Taifa ya Ivory Coast Juni 2 huko Abdijani kujiandaa na mchezo wa awali wa kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia.
Mbali na miamba hiyo ya soka ya Afrika Magharibi Stars iko kundi moja na Gambia na
Morocco.

MAANDAMANO YA SHEREHE ZA UBINGWA SIMBA YALIVYOKUWA


Baadhi ya wachezaji wa Simba SC wakishangilia pamoja na kombe lao wakati wakipita katika mitaa ya jiji la Dar es Salaam leo.
Mashabiki na wapenzi wa Simba SC wakiwa katika maandamano kuelekea katika Ukumbi wa Dar Live kusherehekea ubingwa wa timu yao leo.
Pikipiki zikiongoza msafara huo kuelekea Dar Live.
Maandamano yakipita katika mitaa leo.
Mashabiki wa Simba wakimuenzi kiungo wa timu hiyo, Marehemu Patrick Mafisango aliyefariki katika ajali ya gari hivi karibuni.
Mashabiki wakishangilia wakati wa maandamano hayo.
Wachezaji na mashabiki wa Simba wakipozi na kombe lao.
Mashabiki wa Simba wakiingia ndani ya Ukumbi wa Dar Live tayari kwa sherehe za ubingwa.
(Picha na Issa Mnally /GPL)

MATOKEO MECHI ZA KIRAFIKI ZA KIMATAIFA HADI LEO DUNIA NZIMA

Landon Donovan (10) wa Marekani akimtoka Scott Brown wa Scotland, kulia, kipindi cha kwanza katika mechi ya kirafiki ya kimataifa jana, mjini Jacksonville, Fla. Marekani ilishinda 5-1.

27 May 2012
Fifa Internationals
Tunisia 5 - 1 Rwanda Monastir
Albania 1 - 0 Iran Istanbul
Oman 1 - 1 Lebanon Muscat
Honduras 0 - 1 New Zealand Dallas
USA 5 - 1 Scotland Jacksonville
El Salvador 2 - 0 Moldova Houston


26 May 2012
Fifa Internationals
Algeria 3 - 0 Niger Blida
Norway 0 - 1 England Oslo
Greece 1 - 1 Slovenia Kufstein
Czech Republic 2 - 1 Israel Graz
Netherlands 1 - 2 Bulgaria Amsterdam
Finland 3 - 2 Turkey Salzburg
Cameroon 2 - 1 Guinea Metz
Spain 2 - 0 Serbia St Gallen
Switzerland 5 - 3 Germany Basel
Portugal 0 - 0 Macedonia Leiria
Poland 1 - 0 Slovakia Klagenfurt
Republic of Ireland 1 - 0 Bosnia-Herzegovina Dublin
Brazil 3 - 1 Denmark Hamburg
Mozambique 0 - 0 Namibia Maputo
Burkina Faso 2 - 2 Benin Malabo
Tanzania 0 - 0 Malawi Dar Es Salaam
Costa Rica 3 - 2 Guatemala San Jose


25 May 2012
Fifa Internationals
Morocco 0 - 1 Senegal Marrakech
Belgium 2 - 2 Montenegro Brussels
Croatia 3 - 1 Estonia Rijeka
Russia 1 - 1 Uruguay Moscow


24 May 2012
Fifa Internationals
Georgia 1 - 3 Turkey Salzburg
Japan 2 - 0 Azerbaijan Shizuoka
Peru 1 - 0 Nigeria Lima
El Salvador 2 - 2 New Zealand Houston
Venezuela 4 - 0 Moldova Puerto Ordaz


22 May 2012
Fifa Internationals
Albania 2 - 1 Qatar Madrid
Poland 1 - 0 Latvia Klagenfurt
Egypt 3 - 0 Togo Khartoum
International Friendly
Bayern Munich 3 - 2 Netherlands Munich

No comments: