Sunday, April 8, 2012

VIDIC MSIMU HUU BASI TENA

Vidic
BEKI wa Manchester United, Nemanja Vidic atakuwa tayari kucheza msimu ujao wa 2012-13, hiyo ni kwa mujibu wa kocha wake, Sir Alex Ferguson.
Chifu huyo wa Mashetani Wekundu, amesema kwamba beki huyo wa kati wa Serbia lazima apate muda kuliko kumharakisha kurejea uwanjani baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti, unaomfanyua akose mechi zote zilizobaki za United za kujianda na msimu mpya pia.
Wakati kocha huyo Mscotland anahisi Nahodha wake atakosa mechi za mwanzoni za msimu, kuna alama za kujiuliza kuhusu kiwango cha safu ya ulinzi hivi sasa.
"Ni matumaini – na nafikiri niko sahihi – sisi ni imara sana katika beki ya kat," alisema Sir Alex.
"[Phil] Jones na [Chris] Smalling tumewanunua kwa mikataba ya muda mrefu na wamedhihirisha wanaweza kucheza na nafasi nyingine, ndio, na wakati Vidic atakaporejea, tutakuwa na safu imara sana ya ulinzi,”alisema.
"Hatasafiri nasi katika ziara ya kujiandaa na msimu mpya, lakini atakuwa tayari kucheza mechi za mwanzoni mwa msimu. Kisha nitachagua wawili wa kucheza

No comments: