Sunday, April 8, 2012

JUVENTUS YAPANDA MLIMANI SERIA A

Kocha wa Juve, Antonio Conte
KLABU ya Juventus imeiengua AC Milan kileleni mwa Serie A kwa ushindi wake wa 2-0 dhidi ya Palermo usiku huu.
Mapema Milan ilihitimisha wiki ya machungu kwa kipigo cha 2-1 kutoka kwa vibonde Fiorentina.
Juventus sasa inaizidi pointi moja Milan na Kibibi Kizee hicho cha Turin kina kipaumbele cha kuwafunga na kuwalazimisha sare wapinzani wao hao katika baina yao.
Mabao ya Juventus yalifungwa na Leonardo Bonucci akiunganisha kwa kichwa kona dakika ya 56 na Fabio Quagliarella dakika ya 69 kwa shuti kutoka pembeni baada ya kupokea pasi ya Alessandro Matri.
Ikiwa tayari imekwishafika fainali ya Kombe la Italia, Juventus imeendeleza rekodi yake ya kutofungwa katika mechi 36 kwenye mashindano yote, kipigo cha mwisho wakipata kutoka kwa Parma mwishoni mwa msimu uliopita.

No comments: