Baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa wadau wa tasnia ya korosho Tanzania. |
Na Juma Mohamed, Mtwara
Kampuni ya Golden
Agriculture imeibuka kinara katika ununuzi wa zao la korosho, baada ya
kuwashinda washindani wenzake katika mnada wakwanza wa chama kikuu cha ushirika
cha Tandahimba, Newala Co-operative Union TANECU uliofanyika leo wilayani
Newala.
Mwanasheria
wa Bodi ya Korosho Tanzania CBT mkoani Mtwara, Ugumba Kilasa, ameiambia Juma
News kwa simu kuwa, kampuni hiyo imeshinda kwa bei ya Sh. 3,670 na kuwa kampuni
ilioongoza kwa ununuzi wa bei ya juu katika minada ya leo.
Makamu mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania CBT-Mudhihiri Mudhihiri |
Katika mnada
uliofanyika wilayani Masasi chini ya chama kikuu cha ushirika cha Mtwara,
Masasi Co-operative Union MAMCU, kampuni ya Maviga East Africa imeibuka kinara
kwa kufikia bei ya sh. 3,650 na kuwaacha washindani wake kampuni za Machinga,
Duliva na CDJKL LTD.
No comments:
Post a Comment