Mwenyekiti wa Chademakanda ya kusini, Khamisi Namangaya (kulia) akiwa na katibu wake Philbert Ngatunga na Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Lindi, Latifa Chande. |
Juma Mohamed, Mtwara.
Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kanda ya kusini kimesema kinatarajia kufanya
maandamano na mikutano ya hadhara 8,762 katika mikoa Mitatu ya Mtwara, Lindi na
Ruvuma inayounda kanda hiyo, kuanzia Septemba Mosi mwaka huu.
AKitangaza
maazimio hayo, katibu wa chama hicho kanda ya kusini, Philbert Ngatunga, alisema
hatua hiyo ni kuunga mkono maamuzi ya kamati kuu ya chama hicho ambayo
yametangaza kuanza kufanya maandamano na mikutano ya hadhara ifikapo Septemba
Mosi mwaka huu katika oparesheni ya Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania
(UKUTA), yenye lengo la kupinga kile ilichokiita ukandamizaji wa demokrasia
“Kila ngazi
ya chama ndani ya kanda ya kusini itafanya hilo jambo na tunalisimamia lazima
lifanyike, kwahiyo kwa ujmla wake kuanzia ngazi ya msingi mpaka ngazi ya kanda
pekeyake, kila ngazi itafanya na kwa ujumla kutokana na hesabu ambazo
nimewaambia kutakuwa na jumla ya maandamano na mikutano ya adhara 8,762 kwa hii
mikoa mitatu ya kanda ya kusini..” alisema.
Viongzi wa Chadema kanda ya kusini wakiwa na wabunge wa viti maalumu wa mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma. |
Aidha, chama
hicho kimepingana na kauli za msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Francis
Mutungi, kwamba wamekiuka misingi ya sheria ya vyama vya siasa na kumtaka
azipime kauli zake hizo.
“Tunamshangaa
na tunampinga kauli iliyotolewa na msajili wa vyama vya siasa Jaji
Mutungi..Francis Mutungi, kwakusema kwamba baada ya mwenyekiti (Freeman Mbowe)
kutoa maazimio yale mbele ya waandishi wa habari ameonesha kwamba Chadema
inataka kuleta vurugu, Chadema inakiuka misingi ya sheria za vyama vya siasa..kwahiyo
sisi ile kauli aliyoitoa July 27 Jaji Mutungi msajili wa vyama vya siasa
anatakiwa aipime upya..” aliongeza Ngatunga.
Chama hicho
kimepanga kuanza kuendesha maandamamo pamoja na mikutano ya hadhara nchi nzima katika
kutekeleza oparesheni yake ya Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania (UKUTA),
yenye lengo la kupinga kile ilichokiita ukandamizaji wa demokrasia.
No comments:
Post a Comment