Naibu waziri wa Mazingira, Mhe. Luhanga Mpina (katikati) akiwa katika ziara ya kikazi katika kiwanda cha SBS Mtwara. |
Naibu waziri wa Mazingira, Mhe. Luhanga Mpina, akisikiliza maelekezo kutoka kwa meneja uzalishaji wa kiwanda cha SBS Mtwara, Joseph Wandiba. |
JUMA MOHAMED, MTWARA.
Serikali
imeliagiza Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)
kuhakikisha ndani ya mwezi wanafanya ukaguzi wa viwango vya moshi na maji
katika kiwanda cha kuchakata taka zinazotokana na shughuli za uzalishaji wa
mafuta na gesi cha Supply Base Solution (SBS) mkoani Mtwara, na kujiridhisha
kuwa havina madhara kwa jamii.
Agizo hilo
limetolewa mkoani Mtwara na naibu waziri wa Mazingira, Mhe. Luhanga Mpina,
baada ya kufanya ziara katika kiwanda hicho na kuona namna ambavyo shughuli
zinavyoendeshwa.
“NEMC
wajiridhishe na vipimo vya moshi, wajiridhishe na vipimo vya maji wayapime na
wajiridhishe kwamba yako salama katika viwango vinavyoruhusiwa..kwasababu maji
yale ya kwenye tenki kama tuvyoyaona huwezi sana kuyazuia kutoroka..unaweza
kupunguza lakini huwezi kuyazuia kabisa..” alisema.
Hatua hiyo
ilitokana na katibu tawala wa mkoa wa M
Mmoja wa wafanya kazi wa kiwanda cha SBS Mtwara, akiendelea na majukumu yake. |
Luanda
alisema maelekzo ya kuwataka kuhama yalishatolewa mapema na aliyekuwa naibu
waziri wa Mazingira katika serikali ya awamu ya Nne, Mhe. Ummy Mwalimu wakati
alipotembelea kiwanda hicho pamoja na kusikiliza maoni ya wananchi.
“Kulikuwa na
maelekezo kwamba hawa watu watafute eneo, wahamishe kiwanda..kiwanda ambacho
tunakihitaji kwasababu shughuli za mafuta ndio zinaendelea mkoani Mtwara..”
alisema Luanda.
Kwa upande
wake, meneja uzalishaji wa kiwanda hicho, Joseph Wandiba alisema kuwa hajawahi
kupokea agizo lolote la kuwataka kuondoka eneo hilo, na kudai kuwa atalifikisha
kwa viongozi wa ngazi za juu kwasababu ndio amelisikia kwa mara ya kwanza.
Naibu waziri
huyo anaendelea na ziara yake ya siku tatu mkoani humo ambapo miongoni mwa
maeneo atakayotembelea ni pamoja na kiwanda cha Saruji cha Dangote Industries
Limited na kiwanda cha kuchakata gesi asilia cha Madimba.
No comments:
Post a Comment