|
Mwenyekiti
wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mtwara (MTWAREFA), Athuman Kambi
(katikati) akitoa neno la shukrani baada ya kumalizika kwa uchaguzi.
kulia ni makamu mwenyekiti, Edward Kapwapwa.
|
|
Mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF na mmoja wa wakurugenzi wa timu ya Ndanda Fc ya Mtwara, Mohamed Remtula (Mamu) akipiga kura.
|
|
Wajumbe wakipiga kura.
|
|
Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya MTWAREFA Hussein kingi akiwahusia viongozi wapya chama hicho
|
|
Athuman Kambi akivishwa taji na swahiba wake Ally Mchokoleka baada ya kushinda uchaguzi
|
|
Kizito Mbano akivishwa taji kwa ushindi wa katibu wa MTWAREFA
|
|
Katibu msaidizi Baraka Jamali akiwa na viongozi wenzake wa MTWAREFA baada ya kumalizika uchaguzi
|
|
Edward Kapwapwa akivishwa taji baada ya kuitetea nafasi yake ya makamu mwenyekiti.
|
|
Baadhi ya viongozi wapya wa MTWAREFA wakiwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi.
|
Na Juma Mohamed, Masasi.
CHAMA cha
Mpira wa Miguu Mkoa wa Mtwara (MTWAREFA) kimefanikiwa kupata viongozi wapya
kufuatia kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa chama hicho uliofanyika leo wilayani
Masasi mkoani hapa.
Uchaguzi huo
uliohudhuriwa na wajumbe 30 wa mkutano mkuu, ulitanguliwa na mkutano mkuu ambao
uliendeshwa kwa muda mfupi na mwenyekiti wake Athumani Kambi ambaye baadaye
alijiuzulu kwa ajili ya kugombea upya nafasi yake.
Jumla ya
wagombea 14 walikuwa wakiwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo ambapo
wagombea watano walikuwa wakiwania nafasi tatu za ujumbe wa mkutano mkuu wa
MTWAREFA huku nafasi za mweka hazina, mwakilishi wa vilabu na mjumbe wa mkutano
mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) zikiwa na mgombea mmoja kila
nafasi ambao walipigiwa kura za ndiyo na hapama.
|
Atuman Kambi akivishwa taji baada ya kufanikiwa kuitetea nafasi yake ya mwenyekiti wa MTWAREFA.
|
Nafasi nyingine
ambazo zilikuwa na mgombea mmoja ni katibu mkuu, makamu mwenyekiti na
mwenyekiti huku nafasi ya katibu mkuu msaidizi ikiwaniwa na watu watatu ambao
ni Baraka Jamali, David Paul na Abasi Mkuwaje.
Katika matokeo
ya uchaguzi huo yaliyotangazwa na mwenyekiti
wa kamati ya uchaguzi ya MTWAREFA, Hussein Kingi, yalimfanya Athuman Kambi
kufanikiwa kuitetea nafasi yake kwa kupata ushindi wa kishindo wa asilimia 100
baada ya kupigiwa kura za NDIYO na wajumbe wote 30 wa mkutano huo.
Aidha,
Edward Kapwapwa pia amefanikiwa kuitetea nafasi yake ya makamu mwenyekiti kwa
kupata kura za NDIYO 29 kati ya 30 za wajumbe wote huku kura moja ndio ambayo
ilikuwa ya HAPANA.
Viongozi
wengine waliochaguliwa kihalali kupitia uchaguzi huo watakaoongoza kwa muda wa
miaka mine ni Kizito Mbano ambaye amepata nafasi ya katibu mkuu wa chama kwa
kura za NDIO 29, Baraka Jamali anayekuwa katibu mkuu msaidizi kwa kupata kura
16 na kuwashinda wapinzani wake David Paul kura 9 na Abasi Mkuwaje kura 5.
|
Baraka Jamali akivishwa taji kwa ushindi
|
Nafasi ya
mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF imeendelea kusalia kwa Mohamed Remtula (Mamu)
ambaye amepigiwa kura za NDIO 29, huku nafasi ya mwakilishi wa vilabu ikibakia
kuwa kwa Yahaya Jamali aliyeitetea kwa kupata ushindi wa asilimia 100 kwa
kupata kura za NDIO 30 na Thomasi Mhanga akipata nafasi ya mweka hazina baada
ya kupewa kura 21 na NDIO huku kura 9 zikimkataa.
Nafasi tatu
za wajumbe wa MTWAREFA zilizokuwa zikiwaniwa na wagombea watano na idadi ya
kura zao kwenye mabano, zilienda kwa Hamisi Kangomba (25), Fredrick Nachinuka
(24) na Keneth Kilinga (21).
|
Wajumbe
wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa MTWAREFA wakiwa katika picha ya pamoja
na mkuu wa wilaya ya Masasi, Bernad Nduta baada ya kuwafungulia mkutano
huo.
|
No comments:
Post a Comment