Friday, April 29, 2016

Watendaji halmashauri Mtwara wakumbushwa kwenda na kasi ya JPM.

Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego., akizungumza katika kikao cha uzinduzi wa mradi wa Uimarishaji wa Mifumo katika Sekta za Umma (PS3), utakaotekelezwa katika halmashauri zote za mkoa wa Mtwara.



Wakuu wa wilaya za Masasi, Newala na Nanyumbu, Christopher Maghala {kushoto}, Benard Nduta {katikati} na Sauda Mtondoo.


Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally.




NA Juma Mohamed, Mtwara.

WAKUU wa idara wa halmashauri zote mkoani hapa wametakiwa kwenda na kasi ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Magufuli, katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku ya kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo wanayohitaji.
Akizungumza katika uzinduzi wa mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3), mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, aliwaeleza viongozi hao kuwa wakati huu ni wa kufanya kazi na wenye tabia za kuzembea wanapaswa kujifunza kutokana na yanayowakuta viongozi wengine wenye tabia hizo.

Wajumbe wa kikao cha uzinduzi wa mradi


“Serikali yetu inajitahidi sana kutuwezesha, lakini tunaporudi kwenye maeneo yetu ya kazi kila siku tunakuwa wazamani hatuzaliwi upya, visingizio ni vingi kuliko kazi..basi niombe katika kuendeleza huu mradi wetu na ile ya nyuma basi tuzaliwe upya sisi Wanamtwara, twende na kasi ambayo kwakweli Mhe. Rais wetu anakwenda naye.”
Alisema, siku zote kiongozi na mtendaji bora ni yule ambaye anamuogopa Mungu na kujali masilahi ya anaowaongoza huku yeye mwenyewe akijiweka mwisho, hivyo kuwataka viongozi hao kwenda na dhana hiyo pamoja ile kauli mbiu ya Mhe. Magufuli ya “Hapa kazi Tu” jambo ambalo litasaidia kutoa msukumo katika utendaji.
Aidha, alisemam ujio wa mradi huo utasaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha masuala ya utawala bora ikiwa ni pamoja na kuimarisha mifumo ya mawasiliano, fedha na utendaji ambapo utaifanya jamii kutambua mambo mbalimbali yanayofanywa na viongozi wao.

Mtaalamu wa fedha wa mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3), Abdul Kitula, akizungumza katika kikao cha uzinduzi wa mradi huo katika mkoa wa Mtwara utakaotekelezwa katika halmashauri zote za Mtwara.


Mtaalamu wa fedha wa mradi huo Abdul Kitula, akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa mradi, alisema halmashauri kupitia mradi huo wenye thamani ya dola za Kimarekani Milioni 62, zitanufaika kwa kuimarika mifumo yao katika utawala bora, fedha, rasilimali watu pamoja na mifumo ya utendaji tafiti.
“Changamoto ni nyingi kwa mfano nimesikia CAG (Mkaguzi na dhibiti wa hesabu za serikali) bungeni kwamba halmashauri zetu zimepata hati za mashaka, na kupata hati za mashaka hakutokani na kitu kimoja ni masuala ya kimfumo yapo ndani yake, kwahiyo wakati mradi unatayarishwa kulikuwa na changamoto nyingi ambazo zilionekana..” alisema.

Mkurugenzi msaidizi wa usimamizi wa rasilimali watu katika mamlaka ya seriakli za mitaa katika ofisi ya Rais Tamisemi, Miriam Mbaga.


Naye mkurugenzi msaidizi wa usimamizi wa rasilimali watu katika mamlaka ya serikali za mitaa kutoka ofisi ya rais TAMISEMI, Miriam Mbaga, aliwataka watendaji wa halmashauri kuwa na utayari wa kuupokea mradi huo na kubadilisha fikra zao ili waweze kuendana na mifumo mipya itakayowekwa kupitia mradi huo.

No comments: