Wanachama wa Umoja Mtwara Sacos (UMOSA) wakiwa katika kikao cha kujadili masuala mbalimbali ya kikundi chao. |
Na Juma Mohamed, Mtwara.
WANAWAKE na
vijana mkoani hapa wametakiwa kujiunga na Umoja Mtwara Sacos (UMOSA) ili waweze
kunufaika na mikopo ya gharama nafuu inayotolewa na SACOS hiyo kwa ajili ya
kujikwamua kimaisha na kuacha kuwa tegemezi.
Wakizungumza
na Nipashe, baadhi ya wanawake ambao ni wanachama wa SACOS hiyo, walisema kuwa kikundi
hicho hakina ubaguzi kwa jinsi yoyote lakini kutokana na baadhi ya wanawake
kuwa na woga wa kuthubutu, kimetoa kipaumbele kwao kuhakikisha wanapiga hatua.
Wanachama wa UMOSA |
“Mimi
niwatoe wasiwasi, kikundi hiki hakibagui jinsia ya kike na kiume tena wanawake
tunapewa kipaumbele hata kupata nafasi ya kuwa viongozi ili tuweze kupata ule
ujasiri wa kuweza kusimama lakini pia kusimama kama mwanamke kuondoa ule
utegemezi wa kumtegemea mwanaume..kwahiyo mimi nawashauri waje wajiunge tunapata
elimu tena wanawake tunapata elimu za bure..” alisema Ritha Kiteleki.
Katibu wa
kikundi hicho Evalaiti Matinga, alisema kutokana na hali ya maisha ilivyo kwa
sasa kuna haja ya kushirikiana baina mke na mume katika kutafuta kipato, hivyo
wanawake lazima wabadilike na kuchangamkia fursa kama hizo za kujiunga na
vikundi vitakavyowapatia mikopo ambayo haina masharti magumu.
Alisema
licha ya kuwa na kibarua kinachomuingizia kipato, lakini aliona kuna umuhimu wa
kujiunga na kikundi hicho kwasaabu ameona Mtwara kuna fursa nyingi z kujikwamua
kiuchumi ambazo kama mtu ukiwa na mtaji mzuri unaweza kufanikiwa.
Mwenyekiti
wa SACOS hiyo iliyoanzishwa mwaka jana yenye jumla ya wanachama 26, Clemence
Mwombeki, alisema inalenga kupunguza makali ya maisha kwa wananchi wa Mtwara
ambao kwa wakifanikiwa kuwa wanachama wanaweza kununua hisa kwa bei nafuu.
“Hisa zetu
ni 250,000 ambazo ni kama hisa 10 kwa maana ya kila hisa moja ni sh. 25,000..SACOS
hii inalenga kupambana na umasikini na imekuwa tofauti na SACOS nyingine ambazo
zimekuwa zikianzishwa katika maeneo tofauti, hii imeundwa na sheria, kanuni na
katiba yetu..” alisema.
No comments:
Post a Comment