Mkuu wa wilaya ya Tandahimba, Emmanuel Luhahula. |
VIONGOZI na
watendaji wa vyama vya msingi 49 wilayani Tandahimba mkoani hapa, wamewekwa
chini ya ulinzi mkali na jeshi la polisi kufuatia agizo la mkuu wa wilaya hiyo
Emmanue Luhahula, kutaka wawekwe ndani kutokana na kushindwa kuwalipa wakulima
fedha za malipo ya tatu kiasi cha sh. Bilioni 1.4.
Akizungumza
katika kikao cha pamoja na viongozi na watendaji hao, mkuu wa wilaya alisema
kitendo cha wao kushindwa kuwalipa wakulima fedha hizo inaonesha kuwa wamekula
kwa sababu wanazozijua wenyewe, jambo ambalo linapelekea kuwagombanisha
wakulima na serikali yao.
“OCD hawa
watu hapa hawatoki mpaka kuwe na makubaliano rasmi ya kisheria na bila
kuhusisha chama cha msingi anachokisimamia..ambaye hana utaratibu wa kupata
fedha na wananchi watakaohusika kutoa hiyo hela kwa ajili ya kura maua na wao
tukiwapata tunawaweka ndani..kwasababu tunaongeza mzigo, unakwepa 100 unalipa
200 unakwepa 10 unalipa 20 hatuwezi tukaendesha wilaya hautwezi tukaendesha
serikali kwa mfumo huo..” alisema.
Aliwataka
viongozi hao kuhakikisha walipa fedha hizo ndani ya wiki moja huku akimwagiza
kaimu Kamanda wa Polisi wa Wilaya hiyo ASP Faki Saidi, kutowaachia watuhumiwa
hao mpaka walipe fedha hizo na atakae shindwa apelekwe gerezani wilayani
Newala.
Kaimu meneja
wa chama cha ushirika cha Tandahimba, Newala Cooperative Union (TANECU), Hassan
Chipyangu, alisema kwa upande wao walitekeleza wajibu wao wa kukusanya korosho
kutoka kwa vyama vya msingi na kisha kuzipeleka mnadani na kuziuza ambapo pesa
za mauzo hayo zinalipwa kwenye akaunti za vyama vya msingi.
“Sasa
kwanini vyama vya msingi hawajalipa malipo kwa wakulima waliobaki nafikiri
majibu watakuwa nayo wenyewe..kwa upande wa usambazaji wa fedha sisi
tunawajibika kuchukua fedha kwenye akaunti ya chama husika kupelekea kwenye
chama husika pia baada ya chama husika kutuandikia hundi ya kututaka sisi
kuchukua pesa yake kwenye akauanti yake na kupeleka kwenye akaunti ya chama cha
msingi..” alisema.
Akitoa
ufafanuzi juu ya fedha anazodaiwa kiasi cha sh. Milioni 88, kiongozi wa chama
cha msingi cha Mtoi AMCOS, Abdallah Mtoi, alisema fedha hizo ziliingizwa katika
mikopo wakati wa uongozi uliopita kabla yake.
“Kiongozi
aliyekuwepo nyuma yangu kwenye malipo ya bonus (ziada), alisema kwamba zimebakia
Tani 21 kwenye bango lake na tani hizo aliweka tu hewa hakujua kama msimu wa
2012/20123 hakujua kama kuna matatizo fulani yalijitokeza..” alisema.
`
No comments:
Post a Comment