Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally, akisalimiana na Nahodha wa Ndanda Kigi Makassy kabla ya kuanza kwa mchezo wao na Kagera |
Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally, akisalimiana na mchezaji wa Kagera Sugar. |
Wachezaji wa Ndanda Fc wakishangilia bao la pili baada ya kuifunga Kagera 2-0 |
Jackson Chove akitoka kushangilia bao |
Na Juma Mohamed, Mtwara.
TIMU ya soka
ya Ndanda Fc ya mkoani hapa imeendelea kuwapa raha mashabiki wake baada ya jana kuibugiza Kagera Sugar mabao 2-0 katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara
uliofanyika katika uwanja wa Nangwanda Sijaona, na kushuhudiwa na mkuu wa
wilaya ya Mtwara, Fatma Ally.
Ushindi huo uliotakana na mabao mawili ya dakika za 75 na 79 ya mshambuliaji tegemeo wa
timu hiyo Atupele Green, unakuwa ni wa pili mfululizo baada ya wiki iliyopita
kuisambaratisha Mwadui Fc ya Shinyanga mabao 2-1 katika uwanja huo na sasa
kufanikiwa kufikisha alama 33 katika msimamo wakiwa nafasi ya Nane.
Mchezo wa jana uliochezeshwa na mwamuzi Endrew Shamba kutoka mkoani Pwani, ulikuwa ni
wakushambuliana zamu kwa zamu katika kipindi cha kwanza ambacho kilimalizika
kwa suluhu huku Ndanda wakikosa kutumia nafasi kadhaa walizozipata langoni mwa
Kagera.
Kiungo wa Ndanda Fc, Bryson Raphael akijaribu kumtoka mchezaji wa Kagera Sugar. |
Kipindi cha
pili Ndanda walionekana kuubadilisha mchezo na kucheza kwa kasi ambapo mwalimu
Malale Hamsini alifanya mabadiliko ya kuwapumzisha Salum Minelly na Bryson Raphael
na nafasi zao kuzibwa na Ahmad Msumi na Omega Seme huku mwalimu Adolph Rishard
wa Kagera akimpumzisha Ramadhani Kipalamoto ambaye alimpisha Rashid Simba.
Mabadiliko hayo
yaliinufaisha Ndanda ambao walijipatia mabao mawili ya haraka yakipachikwa na
Atupele ambaye alizitendea haki krosi za Bryson Raphael na Kigi Makassy ambapo
mpaka dakika zote 90 zinamalizika ni Ndanda ndio waliibuka wababe kwa ushindi
huo wa 2-0.
Bryson Raphael, akishangilia bao la Ndanda Fc katika mchezo wao dhidi ya Kagera walioibuka na ushindi wa 2-0 |
Kimsingi,
Ndanda haijawahi kupoteza mchezo wowote mbele ya mkuu wa wilaya katika mechi
zote tatu alizohudhuria katika mzunguko wa pili wa VPL ambapo mchezo wa kwanza
ulikuwa dhidi ya Prisons uliomalizika kwa suluhu ya 0-0 kabla ya kuwashuhudia
wakiiangamiza Mwadui 2-1 na hapo jana kuigalagaza Kagera 2-0.
Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally, akisalimiana na golikipa wa akiba wa Ndanda, Jackson Chove kabla ya kuanza kwa mchezo wao na Kagera |
Baada ya
mchezo huo, Juma News ilifanikiwa kuzungumza na
walimu wa timu zote mbili kutaka kujua tathmini yao, ambapo mwalimu wa Kagera
Sugar, Adolph Rishard alisema timu yake ilijaribu kutengeneza nafasi kadhaa
lakini wachezaji hawakuweza kuzitumia huku wapinzani wao wakitumia makosa
mawili yaliyofanywa na wachezaji wake na kuweza kupata ushindi.
Jackson chove na Kigi Makassy |
Kuhusu mustakabali
wa timu yake katika kusalia au kushuka daraja katika ligi kuu, alisema bado
wanayo nafasi ya kuweza kupigania kubaki kwasababu wana michezo mitatu ambayo
watacheza nyumbani hivyo anatarajia kupata matokeo mazuri.
Mussa Mbaya, ambaye ni kocha msaidizi wa Ndanda Fc, alisema siri ya mafanikio ambayo yanapatikana kwa timu yake ni umoja ulipo baina ya wachezaji, benchi la ufundi, viongozi na mashabiki ambao wamekuwa wakiunga mkono timu yao hata pale inateleza na kukosa matokeo.
alisema, katika mchezo huo kwa mara ya kwanza walilazimika kumtumia kijana wao waliompandisha kutoka kikosi cha vijana wa Under 20, Riphati Msuya, ambaye alionesha kiwango kizuri na kuwaondoa hofu mashabiki na wadau wengine ambao walimuona kwa mara ya kwanza akivaa jezi ya Ndanda.
"Ukiangalia mchezo wa leo kwenye 'Sub' tulikuwa na watu watatu tu wachezaji wengi ni majeruhi, na tumesajili wachezaji 21 na kama ukiangalia leo tumechezesha mchezaji mdogo kuliko wote nafikiri katika msimu wa ligi kuu..watu wengi hawakuamini kama anaweza kucheza lakini amecheza kwa dakika zote 90.."
Mussa Mbaya, ambaye ni kocha msaidizi wa Ndanda Fc, alisema siri ya mafanikio ambayo yanapatikana kwa timu yake ni umoja ulipo baina ya wachezaji, benchi la ufundi, viongozi na mashabiki ambao wamekuwa wakiunga mkono timu yao hata pale inateleza na kukosa matokeo.
alisema, katika mchezo huo kwa mara ya kwanza walilazimika kumtumia kijana wao waliompandisha kutoka kikosi cha vijana wa Under 20, Riphati Msuya, ambaye alionesha kiwango kizuri na kuwaondoa hofu mashabiki na wadau wengine ambao walimuona kwa mara ya kwanza akivaa jezi ya Ndanda.
"Ukiangalia mchezo wa leo kwenye 'Sub' tulikuwa na watu watatu tu wachezaji wengi ni majeruhi, na tumesajili wachezaji 21 na kama ukiangalia leo tumechezesha mchezaji mdogo kuliko wote nafikiri katika msimu wa ligi kuu..watu wengi hawakuamini kama anaweza kucheza lakini amecheza kwa dakika zote 90.."
Aidha,
mfungaji wa magoli ya mchezo huo Atupele Green, alionesha kufurahishwa na kitendecho
kufunga magoli mawili katika mchezo huo ambayo yamemfanya sasa kufikisha magoli
10 katika michezo yote aliyochezea Ndanda msimu huu.
Kutokana na
kufikisha idadi hiyo ya mabao hadi sasa, mchezaji huyo aliyesajiliwa akitokea
Kagera Sugar msimu uliopita, anaonekana kupata mafanikio mara mbili ya yale
aliyopata akiwa na Kagera kwasababu huko alimaliza msimu akiwa na jumla ya
magoli Matano pekee.
“Kiukweli
nilikuwa na hamu sana ya kuifanya timu iwe salama katika kipindi hiki na ndio
maana nimejitolea nimejituma na mwenyezi Mungu amenisaidia nimeweza kufunga
magoli mawili namshukuru sana..sasa hivi nina magoli 10 kiukweli mimi ‘Striker’
na nimejitambua nimejua kazi ya ‘Striker’ ni kufunga, ili uweze kuuzika na uwe
na maisha bora lazima ufunge magoli..” alisema.
Kiungo wa Kagera Sugar, Erick Kyaruzi akimtoka mshambuliaji wa Ndanda Fc, Atupele Green. |
Alisema,
malengo yake katika mechi tatu zilizobaki ni kuweza kufunga angalau magoli
matatu huku akihitaji goli moja kwa kila mechi ili afikishe idadi ya magoli 13 na
kwamba anatarajia kutimiza malengo hayo.
Baada ya
mchezo wa leo, Kagera wanasalia katika nafasi ya 12 wakiwa na alama 25 katika
michezo 27 waliocheza, huku Ndanda Fc wakirejea katika nafasi ya Nane baada ya
kufikisha alama 33 katika michezo 27 waliocheza.
Ndanda watakuwa
na mapumziko ya takribani wiki mbili kabla ya kukutana tena Bagamoyo mkoani
Pwani kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wao dhidi ya JKT Ruvu utakaofanyika Mei
7 mwaka huu katika uwanja wa Mabatini, huku Kagera wakiwasubiri Azam siku hiyo
hiyo huko Kaitaba mkoani Kagera.
Ligi hiyo
itaendelea tena kesho kwa mchezo mmoja utakaopigwa katika uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam pale Simba Sc watakapowakaribisha Toto Africans ya Mwanza.
Matokeo ya mechi nyingine za vpl hii
leo:
Yanga 1-0
Mtibwa
Coastal
Union 1-0 JKT Ruvu
No comments:
Post a Comment