Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally, akitoa hotuba kwa wahitimu katika chuo cha uwalimu cha Montessori, Mtwara |
Wahitimu wa katika chuo cha uwalimu cha Montessori, Mtwara. |
Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally, akimkabidhi cheti cha uhitimu mmoja wa wahitimu wa chuo cha uwalimu cha Montessori, Mtwara. |
Na Juma Mohamed, Mtwara.
MADAKTARI
nchini wametakiwa kuacha tabia za kufoji vyeti vinavyothibitisha magonjwa
hatari kwa baadhi ya walimu wanaokwepa kwenda kufanya kazi vijijini kwa kisingizio
cha kuugua, na kutaka wapangiwe kufundisha katika shule za mijini.
Akizungumza katika
maafali ya chuo cha Uwalimu cha Montessori mkoani hapa, mkuu wa wilaya ya
Mtwara, Fatma Ally, alisema walimu wengi wanaopangia ajira vijijini wamekuwa na
visingizio vingi ambavyo vinalenga kukwepa kwenda kufundisha huko na kupelekea
mahitaji ya walimu katika shule za vijijini kuwa makubwa.
Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally |
“Unaweza
ukapokea cheti cha kuonesha kwamba huyu mtu anaugonjwa wa hatari, tujue pia
kuna mungu, unaweza ukawa unajiombea maana kama unafoji cheti unasema mimi
naumwa kitu fulani siwezi kukaa sehemu ya mbali na hospitali Mungu anasikia unaweza
ukajikuta unajiombea dua mbaya mwenyewe..” alisema.
Aliongeza kuwa,
waajiriwa wengi walioko mijini walianzia huko huko vijijini na wakati mwingine
hata teknolojia ya mawasiliano inakuwa ngumu lakini ni uvumilivu na moyo wa
kujito kufanya kazi kwa bidii ambapo baadae wameweza kuhamishiwa katika vituo
vya mijini.
Burudani ya aina yake |
Kuhusu suala
la kuchelewa kwa ajira za walimu ambalo liliwasilishwa na wahitumu kupitia
risala yao, mkuu wa wilaya aliwaomba kuwa wavumilivu na kusema kuwa mambo
mazuri hayataki haraka na kuwahakikishia kuwa sekta ya elimu ajira zipo hata
kama zinachelewa.
Mwenyekiti wa
bodi ya ushauri ya chuo, Francis Kasoyaga, alisisitiza juu ya nidhamu kwa
wahitimu hao ambao jumla yao ni 33 kwa daraja la 3 A, ambayo wamedumu nayo kwa
kipindi chote walichokaa katika chuo hicho kilicho chini ya shirika la kidini
la Mkombozi.
Mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya chuo cha uwalimu cha Montessori, Mtwara, Francis Kasoyaga, akiwahusia wahitimu wa chuo hicho juu ya namna ya kwenda kuishi waendako. |
“Mumehitimu
katika chuo ambacho kinaendeshwa maadili ya kiroho lazima tuoneshe tabia zetu
kuwa ni tofauti na za wale ambao wametoka katika vyuo vingine, kila mtu
akikuona ajue kabisa kwamba huyu ametoka katika chuo cha Montessori kwa matendo
yako..” alisema Kasoyaga.
Chiku
Jamuhuri, ambaye ni miongoni mwa waliohitimu chuoni hapo, aliahidi kwenda
kupambana na changamoto zozote zinazowakabili walimu na kwenda kuyafania kazi
yale yaliyosisitizwa na mkuu wa wilaya katika hotuba yake.
Aidha,
aliishauri serikali kuona umuhimu wa kuboresha masilahi ya walimu hasa
mishahara pamoja na kuboresha miundombinu ya kuwawezesha kutoka sehemu moja
kwenda nyingine kupata mahitaji mbalimbali.
No comments:
Post a Comment