Katibu wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (CCC), Mary Shao, akifafanua jambo. |
Na Juma Mohamed, Mtwara.
WATOA huduma
za nishati na maji, usafiri wa anga, huduma za mawasiliano na huduma za usafiri
wa nchi kavu na majini, wametakiwa kuhakikisha wanakuwa na mfumo thabiti wa
utoaji taarifa zinazowahusu wateja wao kila wakati taarifa hizo zinapohitajika
au kupatikana.
Akizungumza
kwa niaba ya kaimu mwenyekiti wa Jukwaa la Watumiaji (TCF), Thomas Mnunguli,
katibu mtendaji wa Baraza la Ushauri la EWURA, Goodluk Mmari, alisema wakati
Tanzania ikielekea katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya haki za mtumiaji
ambayo kilele chake ni Machi 15 mwaka huu, watoa huduma hizo wanapaswa
kutafakari mifumo ya utoaji taarifa wanayoitumia na kujipima ili kuona kama
inakidhi mahitaji ya sasa kwa wateja.
Alisema,
pamoja na ukweli kuwa uhitaji wa taarifa unaongezeka miongoni mwa watumiaji
siku hadi siku, bado utoaji taarifa kwa watoa huduma unakumbwa na changamoto
nyingi zikiwamo kutotoa taarifa kabisa ikiwa ni pamoja na katizo la huduma na
ucheleweshwaji au kuahirishwa kwa safari.
Mhandisi Goodluck Mmari |
“Siku za
hivi karibuni tumeshuhudia watoa huduma kwa mfano wanatangaza kuwepo kwa katizo
la umeme kuanzia muda fulani hadi muda fulani lakini watoa huduma hawa
hawazingatii kilichotolewa katika taarifa, mara nyingi utekelezaji wa taarifa
hizo haufuatwi kabisa..au wakati mwingine hakuna taarifa kabisa inayotolewa.”
Alisema.
Aidha,
aliongeza kuwa, mbali na kuwa na mikataba ya huduma kwa wateja, watoa huduma
wote wa huduma zinazodhibitiwa wanapaswa kuwa na mkakati wa mawasiliano ambao
pamoja na mambo mengine, utaainisha njia zitakazotumiwa na watoa huduma katika
utoaji wa taarifa kwa wadau wao ili kuharakisha usambaji wa taarifa kwa lengo
la kuwafikia wahusika kwa haraka zaidi.
Aliwaasa
wakazi wa manispaa ya Mtwara na vitongoji vyake hususani kwa makundi
yatakayowakilisha wakazi wa mkoa huo, kushiriki kikamilifu katika semia za
uelimishaji zilizoandaliwa kwa makundi hayo na kuwaomba kuwa mabalozi wazuri wa
kusambaza elimu kwa watumiaji wanaotumia huduma na bidhaa zinazodhibitiwa.
Mary Shao |
Kwa upande
wake, katibu mtendaji wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za
Mawasiliano (CCC), Mary Shao, alisema Tanzania pamoja na nchi nyingine za
Kiafrika ziko nyuma katika suala la kutekeleza haki za watumiaji kwasababu nchi
nyingi baada ya uhuru, serikali ndio ilikuwa mtoa huduma huku sekta binafsi
zilianza kuingia katika kutoa huduma mwishoni mwa miaka ya 80.
“Kuwepo kwa sekta
binafsi ambazo pia ni mzuri kwa uchimi na pia zinaleta ‘product’ nyingi kwenye
soko, kwa wale ambao wamezaliwa nyuma kidogo watakumbuka kuwa zamani simu
ilikuwa ni TTCL pekeake, ukija kwenye basi utakuta UDA pekeake kwenye maji
hivyo hivyo sasa inapokuwa watoa huduma ni wengi ‘product’ zinakua nyingi..”
alisema.
No comments:
Post a Comment