Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Mfaume Juma. |
Na Juma Mohamed, Mtwara.
BODI ya
Korosho Tanzania (CBT), imesema msimu huu uliomalizika mwezi Januari ulikuwa na
mafanikio makubwa ukilinganisha na misimu mingine, ambapo kwa mara ya kwanza
wamefanikiwa kutoa leseni kwa wanunuzi 120,000 kununua zao hilo.
Hayo
yalielezwa jana mkoani hapa na mkurugenzi mkuu wa Bodi hiyo, Mfaume Juma,
wakati akifanya mahojiano katika kituo kimoja cha redio kwa ajili ya kuelezea
tahmini mzima ya zao hilo kwa msimu wa 2015/2016.
Alisema
mafanikio mengine ambayo yameonekana katika msimu huu uliomalizika ni kuboreka
kwa bei ambapo kwa mujibu wa mkutano wa wadau uliofanyika mwezi Agosti mwaka
jana mkoani Lindi, bei dira ilikuwa ni sh. 1,200 huku malipo ya kwanza ikiwa ni
sh. 900.
“Mkutano ule
ambao unawakutanisha wadau mbalimbali wa zao la korosho wakiwamo wakulima
wenyewe, ndio unapanga mikakati na hata bei dira kwa msimu husika..na msimu huu
bei dira ilikuwa sh. 1,200 huku malipo ya kwanza yalikuwa ni sh. 900..na niseme
tu kwamba kuna sehemu minada ya korosho iliuzwa mpaka sh. 2,900, hii ni
kuonesha korosho msimu huu ulikuwa nzuri..” alisema.
Alisema,
pamoja na kuwepo kwa changamoto kadhaa ikiwamo ya wanunuzi wasio rasmi maarufu
kama Kangomba, lakini vyama vya msingi vilijitahidi kukusanya korosho kwa wingi
na hata uuzaji ulikuwa mzuri kiasi cha kuwafanya wakulima wapate malipo yao
vizuri na kwa wakati tofauti na misimu mingine.
Aidha,
aliwataka wakullima kuachana na kuuza korosho kwa Kangomba ambao ni mfumo
unaodidimiza kipato chao, kwani hata wao wanaonunua kwa mtindo huo wengine
wanauza katika maghala yaleyale ya vyama vya msingi ambayo wakulima wangeweza
kuuza korosho zao huko kwa bei nzuri tofauti na ile wanayoipata kwa Kangomba.
“Wakilma
wanapaswa kupunguza au kuacha kuuza korosho kwa kangomba kwasababu wanadidimiza
kipato chao..kwanza suala la kangomba ni uvunjifu wa sheria na mamlaka zote
zinafaa kushirikiana katika kuhakikisha tunalimaliza hili..na mtu wa kwanza
kushughulikia hili ni mkulima mwenyewe..” alisema.
Alisema
mafanikio hayo katika msimu huu ni kutokana na sehemu kubwa zinazolima zao hilo
kutekeleza mfumo wa stakabadhi ghalani huku mkoa wa Pwani ukiwa umetekeleza kwa
mara ya kwanza msimu huu baada ya kuwa nje mfumo huo kwa miaka kadhaa iliyopita.
Aliwaponngeza
Mnazimmoja kupitia chama chao cha msingi kwa kuwa wawazi kwa wakulima wao na
kujitahidi kutoa mchanganuo wa kila hatua inayoendelea katika mchakato wa
kukusanya na kuuza korosho na kisha kubandika sehemu za wazi ili kila mkulima
aone kiasi alichokusanya na kuuza.
Alivishauri
vyama vya msingi kujitahidi kutokopa fedha benki jambo ambalo linapeleka
kumlipa mkulima kidogokidogo na kumfanya hasione manufaa ya zao hilo na baadala
yake wajitahidi kulipa fedha hzio kwa pamoja.
No comments:
Post a Comment