Mmoja wa mafundi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Mtwara, akitekeleza majukumu yake. |
Na Juma Mohamed, Mtwara.
WANANCHI wa
mikoa ya Mtwara na Lindi wametakiwa kujiandaa na kupanda kwa gharama za kuvuta
umeme majumbani (Service line) zitakazofikia kiasi cha sh. 177,000 kama maeneo
mengine kutoka sh. 99,000 ya sasa.
Akizungumza
juzi ofisini kwake, Mhandisi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa
Mtwara, Daniel Kyando, alisema punguzo hilo ilikua ni ofa maalumu ambayo
ifikapo Machi 31 mwaka huu itafikia mwisho, hivyo watakohitaji kuunganishiwa
umeme baada ya hapo watalipia gharama halisi.
“Na hii
ilikuwa ikiongezeka kwasababu ulikuwa ni mpango wa mwaka mmoja toka mwaka 2012
na ilikuwa iishe mwaka 2013, lakini kutokana na ‘situation’ iliyokua Mtwara
ikawa inaongezeka na wateja wengi Mtwara walikua bado hawajaunganishiwa umeme
lakini sasa hivi maeneo yaliosambazwa umeme ni mengi sana kupitia miradi ya REA..”
alisema.
Fundi |
Alisema
tangazo hilo ni kwa wananchi wote wa mikoa hiyo isipokua wale ambao wanapata
punguzo kutokana na kupitiwa na mradi wa bomba la gesi asilia ambao wanalipia
sh. 27,000, ambapo wao ofa yao itamalizika baada ya mradi huo kukamilika.
Aidha, aliwaondoa
hofu wananchi ya Mtwara kutokana na hali ya kukatika kwa umeme mara kwa mara
inayoendelea na kudai kuwa hali hiyo inatokana na marekebisho ya miundombinu
ikiwamo nguzo pamoja na matengenezo makubwa ya mtambo mmoja ambao uliharibika
kutokana na kuanguka kwa nguzo.
Mhandisi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Mtwara, Daniel Kyando, akimuhoji mkazi wa kata ya Chikongola ambaye nyumba anayeishi ilibainika kutumia umeme wa wizi. |
“Hilo zoezi
la kuzipitia nguzo hua linafanyika mara kwa mara lakini historia inaonesha
kwamba suala la maintenesi kwenye mkoa wetu wa Mtwara kuna kipindi hapo nyuma
halijafanyika kwa muda mrefu sana kwahiyo madhara yake ndio tunayaona sasa..unajua
kama unakaa miaka miwili au mitatu hujabadilisha nguzo madhara yake ndio
yanakuja sasa hivi nguzo nyingi zinaanguka kwa wakati mmoja..” alisema.
Alisema,
wananchi wasiwe na wasiwasi kwani huduma hiyo itarejea katika hali yake ya
kawaida ndani ya wiki hii kwasababu vifaa vilivyokuwa vikihitajika kwa ajili ya
matengenezo ya mtambo huo tayari vimewasili.
No comments:
Post a Comment