Katibu tawala wa mkoa wa Mtwara, Alfred Luanda, akihutubia katika kilele cha siku ya Kimataifa ya haki za mtumiaji ambayo Kitaifa imefanyika mkoani Mtwara. |
Baadhi ya wadau kutoka katika taasisi mbalimbali mkoani Mtwara walioshiriki katika maadhimisho ya kilele cha siku ya Kimataifa ya haki za mtumiaji yaliofanyika Kitaifa mkoani Mtwara. |
Katibu tawala wa mkoa wa Mtwara, Alfred Luanda, akihutubia katika kilele cha siku ya Kimataifa ya haki za mtumiaji ambayo Kitaifa imefanyika mkoani Mtwara. |
Na Juma Mohamed, Mtwara.
WATUMIAJI wa
bidhaa mbalimbali zinazodhibitiwa nchini wameshauriwa kudai risiti za manunuzi au
huduma, ambazo zitawasaidia kudai wajibu wao pindi inapotokea tatizo wakati wa
matumizi ya bidhaa au huduma alizopatiwa.
Wito huo
ulitolewa mkani hapa juzi na katibu tawala wa mkoa wa Mtwara, Alfred Luanda,
wakati wa kuhitimisha siku ya Kimataifa ya maadhimisho ya haki za mtumiaji,
yaliyofanyika Kitaifa mkoani hapa katika ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo katika
Chuo cha Uwalimu Mtwara (TTC).
Alisema
mtumiaji anayefahamu haki na wajibu wake ana nafasi kubwa ya kuhakikisha
hadhurumiwi anapofanya manunuzi ya bidhaa sokoni na maeneo mengine
ukilinganisha na yule ambaye hafahamu wajibu wake.
“Mtumiaji
atakaefahamu umuhimu wa kudai risiti na akafanya hivyo kwa kila manunuzi
anauwezekano mkubwa wa kuanzisha malalamika endapo atatendewa visivyo katika
shughuli zake za kununua bidhaa katika soko..” alisema na kuongeza:
“Mtumiaji
atakaetumia taarifa za upakiaji salama wa mizigo katika vyombo vya usafirishaji
atakua na uhakika wa mizigo yake kufika salama kuliko asiye na taarifa hizo..”
aliongeza.
Aliwataka watumiaji
kuwa na utaratibu wa kujisimamia wakati akifanya manunuzi kwani kwa kufanya
hivyo watakuwa makini katika kuhakikisha wanapata wajibu wao kuliko yule ambaye
anasubiri serikali imsimamie.
Kwa upande
wake, katibu mtendaji wa baraza la ushauri la Mamlaka ya Usimamizi wa Huduma za
Usafiri wa Nchikavu na Majini (SUMATRA), Dkt. Oscar Kikoyo, alisema kabla ya
kilele cha maadhimisho hayo, kulikuwa na kazi za uelimishaji kwa watumiaji
iliyokuwa ikifanywa na mabaraza yanayounda Jukwaa la Watumiaji.
Kaimu mwenyekiti wa Jukwaa la Watumiaji Tanzania (TCF), Thomas Mnunguli akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya haki za mtumiaji. |
Alisema,
miongoni mwa changamoto walizozipokea kutoka kwa watumiaji ni maswali juu ya
kukatika kwa umeme mara kwa mara, miundombinu mibovu ya maji na makato ya kila mwezi
katika huduma za maji na umeme (Service Charge) na kudai kuwa hakuna taarifa
zinazotolewa kwa watumiaji juu ya changamoto hizo.
Alisema,
kupitia mabaraza hayo, waliweza kutoa elimu kwa watumiaji juu ya namna ya kudai
haki zao za kupata taarifa kwa huduma wanazopewa kutoka katika kampuni au
mashirika mbalimbali.
“Kazi kubwa
tunayoifanya ni kutoa elimu kwa mtumiaji kwamba yeye mwenyewe aweze kudai haki
yake, mojawapo ya haki anayoweza kudai ni haki ya kupewa taarifa, kwamba ok
kuna huduma hii, je mtumiaji ana taarifa za kutosha kuhusu huduma Fulani..”
alisema Kikoyo.
No comments:
Post a Comment