Na Juma Mohamed, Mtwara.
SERIKALI
mkoani hapa imesema inamatumaini makubwa kwa wananchi wake kuwa watanufaika na
shughuli za uwekezaji zinazoendelea kufanyika kwa kujishughulisha na njia
mbalimbali za kujiingizia kipato kitakachotokana na fursa za uwepo wa
rasilimali za mafuta na gesi asilia.
Akizungumza
kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego katika zoezi la uzinduzi wa
kituo kikubwa cha uwekezaji cha kuhifadhia vitendea kazi mbalimbali
vitakavyotumiwa na makampuni yanayofanya shughuli za utafiti na uchimbaji wa
mafuta na gesi, katibu tawala wa mkoa wa Mtwara, Alfred Luwanda, alisema mahitaji
ya bidhaa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuku na mbogamboga yatakuwa makubwa
hivyo ni fursa kwa wananchi kuweza kuzitumia.
“Tunapoona
makampuni yanakuja kwa wingi, hawa watahitaji chakula, watahitaji mbogamboga,
watahitaji matunda na vingine..sasa hivi vitu kama havitokuwepo katika maeneo
haya watakaonufaika watakuwa ni watu wengine..kwahiyo sisi kama mkoa tuligemea
kuona wawekezaji zaidi kutoka nje wakija kuwekeza katika shughuli au masuala
yanayoendana na gesi..” alisema.
Alisisitiza
kwa wadau mbalimbali wa maendeleo kushirikiana katika kuwaandaa wananchi
kifikra na kwa kuwapatia mafunzo mbalimbali yatakayowawezesha kuwa na uelewa
zaidi juu ya namna watakavyonufaika na rasiimali hizo ambazo faida yake
huchukua muda mpaka mwananchi kuanza kuiona.
Kwa upande
wake, mkurugenzi wa Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji (EPZA), Kanali
Mstaafu Joseph Simakalia, alisema kituo hicho kinachojengwa katika eneo hilo
kitatumiwa na makampuni yanayojihusisha na shughuli hizo kutoka katika nchi
zote za Afrika Mashariki na Kati na zile za ukanda wa SADC isipokuwa nchi ya
Angola.
Alisema,
hatua ya kituo hicho kuja kujengwa Tanzania imetokana na makubaliano ya nchi
hizo kutokana na kufanya tathmini ya kupata eneo ambalo litakuwa la katikati
kwa nchi zote na lenye mahitaji muhimu kutokana na shughuli zao ikiwa ni pamoja
na bandari ya uhakika na rasilimali za gesi na mafuta.
‘Kwahiyo
Tanzania imekaa katikati, kwamba tukiweka kituo kikubwa cha kudumu Tanzania
kwamba mahitaji yote yanawekwa pale alafu anaehitaji kwa kiasi anachotaka
anapelekewa ikaonekana ni Tanzania na sehemu yenyewe ni Mtwara, kwasababu
bidhaa nyingi zitakuja kwa bahari na zitasafirishwa majini na Mtwara kuna
bahari alafu vilevile Mtwara yenyewe ina gesi..kwahiyo ni kama Mungu
amependelea Mtwara ina kila sababu ya hicho kituo kiwekwe hapa..” alisema.
Alisema, kwa
uwepo wa lituo hicho, mkoa utanufaika kwa kujiongea makusanyo ya mapato
yatokanayo na bandari kwasabau bandari itatumika zaidi kuliko ilivyo sasa, na
kuongezeka kwa ajira katika bandari hiyo ambayo ndio itatumika kwa meli kubwa
zitakazo beba vifaa hivyo.
Eneo hilo ambalo
ni mali ya EPZA lina ukubwa wa heka 3.5 na kwamba ujenzi wake unatarajiwa
kuanza wiki hii.
No comments:
Post a Comment