Na Juma Mohamed.
MWANAFUNZI
wa kidato cha Tatu katika shule ya sekondari ya Mtwara Ufundi mkoani hapa,
Tawfiq Hamisi (17), amefariki dunia baada ya kukatwa na kiwembe katika mkono
wake wa kulia na mwanafunzi mwenzake Issac Yohana (16).
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo, kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara, Henry Mwaibambe,
alisema kabla ya kifo hicho kulikuwa na ugonvi kati ya marehemu na mtuhumiwa
ambaye ni Isssac anayedaiwa kuficha kiatu cha mwenzie ambapo baada ya mzozano
akaamua kumkata na kiwembe mwnzie chini ya bega lake la kulia.
Alisema tukio
hilo lilitokea usiku wa juzi kuamkia jana majira ya saa Tano usiku, ambapo
marehemu alivuja damu nyingi kuanzia muda huo mpaka alfajiri alipochukuliwa na
kukimbizwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mtwara, Ligula kwa ajili ya
matibabu.
“Kwahiyo
damu ilitoka nyingi sana usiku ule, lakini wale wanafunzi waliogopa kwenda
kuuambia uongozi wa shule wakidhani kuwa ni jeraha la kawaida..lakini kadri
muda ulivyoenda hali ya kijana ikawa inabadilika ndipo walipokwenda kutoa
taarifa kwa uongozi majira ya saa 10 alfajiri kwamba mwenzetu hali yake sio
nzuri kulitokea ugonvi..” alisema.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mtwara, Henry Mwaibambe. |
Alisema,
mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi la polisi kwa upelelezi zaidi huku akibainisha
kuwa kwa mujibu wa sheria za nchi kijana huyo mwenye umri wa miaka 16 ana haki
ya kushitakiwa na kwamba zipo taratibu zinazopaswa kufanywa na jeshi hilo.
“Kwahiyo
huyu kijana mshitakiwa Issac Yohana tunamshikilia, wote ni wanafunzi wa kidato
cha Tatu, tunamshikilia kwa mauaji ya tukio hili na mwili wa marehemu
unafanyiwa uchunguzi pale Ligula na tumeiachia shule kwa taratibu za
kusafirishwa..” alisema.
Aliongeza kuwa
marehemu ni mwenyeji wa mkoa wa Tanga huku mtuhumiwa ni mwenyeji wa wiayani
Newala mkoani hapa, na kutoa wito kwa wanafunzi hasa wanaosoma katika shule za
bweni kuepuka kuchukua maamuzi yenye kuleta madhara kama ilivyo kwa tukio hilo.
Mganga mfawidhi
wa hospitali ya Ligula, dkt. Mdoe Mhuza, alithibitisha kupokelewa kwa mwili wa
marehemu majira ya saa 11 alfajiri na kudai kuwa bado uchunguzi zaidi
unaendelea kwa ajili ya kuweza kubaini chanzo cha kifo chake.
“Kwa taarifa
za awali ni kwamba ilionekana tu ana jeraha kwenye sehemu ya mkono, mpaka
tutapofanya uchunguzi ndipo tutabaini nini kimepelekea mpka anapa umauti..Daktari
wa zamu ambaye alikuwepo kwa zamu ya usiku (Dkt. Benardetha Mwambe) alisema
kwamba walifika kwenye majira ya saa 11 alfajiri..” alisema.
No comments:
Post a Comment