Friday, October 9, 2015

Zoezi la uwekaji jiwe la msingi-PPF PLAZA-Mtwara sasa kufanyika leo

Naibu waziri wa Fedha, Mhe. Adam Malima, akitoa tangazo la kuahirisha shughuli ya uwekaji jiwe la msingi katika jengo la Mfuko wa Pensheni wa PPF (PPF PLAZA), mkoa wa Mtwara jana, baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete, kuchelewa kuwasili mkoani hapa kutokana na kuwa katika ziara ya kiserikali nchini Msumbiji.

Adam Malima


Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wakiwa katika viwanja vya jengo la PPF Plaza mkoa wa Mtwara, wakimsubiri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi jengo hilo ambalo ujenzi wake unaendelea.





 Na Juma Mohamed.

Shughili ya uwekaji wa jiwe la msingi katika jengo la uwekezaji la Mfuko wa Pensheni wa PPF (PPF PLAZA) mkoani Mtwara, ambayo ilikuwa ifanywe na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete, ilishindwa kufankiwa jana kutokana na Rais kuchelewa kuwasili mkoani hapa.

Akitoa tangazo la kuahirishwa kwa shughuli hiyo, Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Adam K. Malima, alisema Mhe. Rais alichelewa kuwasili kutokana na kuwa na ziara ya kiserikali nchini Msumbiji, ambapo hata hivyo aliwasili usiku majira ya saa 1.

Adam Malima

 Aidha, shughuli hiyo sasa inatarajiwa kufanyika leo Oktoba 11 kabla ya Mhe. Rais kwenda katika miradi mingine iliyopo manispaa ya Mtwara Mikindani kisha kumalizia ziara yake katika halmashauri ya wilaya ya Mtwara, ambapo huko anatarajiwa kuzindua kiwanda cha kuchakata gesi asilia kilichopo Madimba na baadaye kiwanda cha Saruji, cha Dangote, kilichopo Msijute.


No comments: