Na Juma Mohamed
MAKAMU
mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Severina Mwjage, amewataka vijana na
wananchi kwa ujumla kujitokeza kwa wingi Oktoba 25 kupiga kura za mabadiliko,
na kuacha kuhofia kuibiwa
Akizungumza
jana katika mkutano wa hadhara wa kunadi sera na kuwaombea kura wagombea Urais,
Ubunge na Udiwani wa jimbo la Mtwara vijijini, uliofanyika katika kata ya
Mahurunga, alisema uwezekano huo haupo kutokana na kuwepo kwa viongozi
mbalimbali ambao awali walikuwepo CCM kabla ya kuingia upinzani.
Severina Mwaijage |
Aidha, aliwataka
wananchi kuwapiga vita na kuto wathamini mabalozi na wenyeviti wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) kwasababu hawatambuliki kikatiba na kwamba wamewekwa kwa ajili
ya kuuhujumu upinzani na kwamba mwisho wa uwepo wao ni mwezi Oktoba mwaka huu.
Alisema,
kumekuwa na tabia zinazofanywa na viongozi hao za kuwashawishi wananchi
wasihudhurie mikutano ya vyama vya upinzani pamoja na kuwapa vitisho, jambo
ambalo amelikemea vikali na kuahidi kuwashitaki watakaobainika kufanya vitendo
hivyo.
“Kama leo
nafikiri umeona kule Nanyati..watu wanapenda kuja katika mikutano lakini
wametueleza mapema kwamba balozi wa CCM na mwenyekiti jana usiku (juzi)
walipita kila nyumba kuwazuia watu wasiende kusikiliza, kusikiliza sio ndio
kuchagua..wasikilize sera za kila chama kwasababu kila chama kinauza sera
zake..” alisema.
Alisema,
kutokana na mwamko wa kisiasa walionao vijana kwa sasa, sio jambo la busara
kuwazuia kwenda katika mikutano na kusikiliza sera za wagombea, kwani viajana
sasaivi wameamka na dio maana wamejitokeza kwa wingi katika zoezi la
kujiandikisha ili waweze kuchagua viongozi wanaowaona wanafaa kutokana na
kuchoshwa na hali ngumu ya kimaisha pamoja na uhaba wa ajira.
Akizungumzia
namna watakavyoweza kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa
halmashauri ya Mtwara vijijini ikiwa ni pamoja na elimu, maji na afya, alisema jambo la kwanza ni
kufumua mikataba ya rasilimali za gesi asilia na mafuta ambayo wanaamini ndio
imebeba utajiri wa wananchi wa maeneo hayo na Kusini kwa ujumla.
“Siku Mhe.
Ngoyai mkimpa kura akashinda, hizi rasilimali zenu, mikataba ya gesi, madini,
mafuta na sijui makolokolo gani wakikataa kuionyesha tutawapeleka mahakamani na
mpaka rais..kwasababu wewe ukiiba kuku hapa unakamatwa na kupelekwa mahakamani
wakati anaeiba mabilioni ya pesa mbona hamfungi..” alisema.
No comments:
Post a Comment