Dkt. Emmanuel Makaidi |
Na Juma Mohamed.
Mwenyekiti
wa chama cha National League For Democracy (NLD) na Mgombea ubunge wa jimbo la
Masasi, Dkt. Emmanuel Makaidi, amefariki dunia akiwa katika hospitali ya
Nyangao, wilaya ya Lindi vijijini mkoani Lindi, kutokana na kuugua shinikizo la
damu.
Kwa mujibu wa Mganga aliyethibitisha kifo chake kutoka katika hospitali hiyo, Dkt. Betram Makota, alisema marehemu alifikishwa hospitalini hapo jana majira ya saa tano asubuhi na mkewe huku hali yake ikiwa mbaya zaidi ambapo alifariki dunia majira ya saa saba mchana.

Alisema,
alianza kuugua siku tatu zilizopita ambapo alienda katika Zahanati moja huko
wilayani Masasi ambako ndiyo nyumbani kwake na kupata matibabu ambayo
ualimsaidia, lakini alivyoamka jana hali ilibadilika na kuishiwa nguvu ndipo
ikaamuliwa akimbizwe hospitalini hapo.
"Aliugua
tangu siku mbili zilizopta, kwahiyo jana walimpumzisha katika Zahanti moja ya
huko wilayani Masasi..baade ikaonekana amepata nafuu, lakini leo asubuhi (jana)
hali ikaanza kubadilika na kuanza kuishiwa nguvu na baadae akakimbizwa hapa
akiwa na baadhi ya ndugu zake wa kiume na mke wake.." alisema.
Alisema
kwa mujibu wa ndugu zake, maiti inasafirishwa leo kwenda jijini Dar es Salaam
kwa ajili ya shughuli za mazishi.
|
No comments:
Post a Comment