Kaimu mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Taifa, Severina Mwijage, akinadi sera za chama katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika jana katika viwanja vya Mashujaa mjini Mtwara. |
Severina Mwaijage |
Wakazi wa Mtwara waliojitokeza katika mkutano wa hadhara wa Chama cha Wananchi CUF wa kunadi sera za ubunge na udiwani uliofanyika jana katika viwanja vya Mashujaa mjini Mtwara. |
Na Juma Mohamed, Mtwara.
JESHI la polisi limetakiwa kutenda haki na usawa katika kutekeleza majukumu yao
katika kipindi hiki cha kampeni na uchaguzi mkuu, ili kuhepuka kuasababisha
kutokea vurugu zitakazopelekea uvunjifu wa amani.
Akizungumza jana mkoani hapa katika mkutano wa hadhara wa kunadi sera uliofanyika katika viwanja vya Mashujaa, kaimu mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Taifa, Severina Mwijage, alisema askari polisi ni marafiki wa raia na ni haki yao kulinda amani na sio kusababisha uvunjifu wa amani.
Alisema zipo tabia kwa jeshi hilo kutumika kwa ajili ya kutetea maslahi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), na kujikuta wanasababisha kutokea kwa vurugu zisizo na msingi kutokana na kuegemea upande mmoja na kuwafanya wananchi kukosa imani nao.
“Tumewatetea mara ngapi sisi wapinzani ili wapate nyumba nzuri, watoto wao wasome vizuri..askari huyo huyo amesomeshwa na baba yake na mama yake kwa pesa ya kusuasua ili mwanawe apate ajira, leo hii amekuwa askari anapelekwa kwenye fulu suti..na nchi yake ni tajiri lakini wakisema mpinzani yuko pale anaharaka ya kumkamata..lakini wenyewe ni masikini na akienda hospitali hakuna dawa ya polisi wala jeshi..” alisema.
Alisema askari wanatakiwa kusoma lama za nyakati na kuto jizuuka na CCM kwa kujua kitaongoza milele kwani chama hicho mwisho wake ni mwezi Oktoba baada ya uchaguzi, na kwamba mkombozi wao atakuwa ni Mhe. Edward Lowassa, ambaye anagombea Urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akiungwa mkono na vyama vya UKAWA.

Naye, mwenyekiti wa CUF wilaya ya Mtwara mjini, Said Issa ‘Kulaga’, alisema baada ya mgombea ubunge wa jimbo la Mtwara mjini kupitia CCM, Mhe. Hasnain Murji, kufungua kampeni zake wiki moja iliyopita, kumekuwa na vitendo vya uonevu vinavyodaiwa kufanywa na jishi hilo.
Alisema kuna vijana wanne wa wafuasi wa CUF wamekamatwa kwa visingizio visivyokuwa na msingi, huku kiongozi wa chama hicho ngazi ya wilaya akiwa amefikishwa mahakamani kwa kudaiwa kumpiga katibu wa vijana wa CCM, jambo ambalo halikuwa la kweli.
“Kosa la kiongozi huyu ni kwenda kumnusuru huyo katibu kwasababu alikuwa anachana mabango ya mgombea Urais, udiwani na ubunge wa UKAWA..ili hasiadhibiwe na wananchi na hatimaye akamfikisha kwenye vyombo vya sheria..lakini polisi walipokea taarifa za daktari wa Ligula (Hospitali ya Rufaa ya Mkoa) aliyedanganya kwamba eti yule ameumizwa sana na kukubali kupeleka kesi polisi..” alisema.
Kwa upande wake, mgombea ubungea wa jimbo hilo kupitia CUF akiwakilisha UKAWA, Maftaha Nachuma, alisema iwapo wananchi watamchagua kuwa mbunge, ataungana na Mhe. Lowassa kutetea maslahi ya zao la korosho kwa kuhakikisha wanaondoa mfumo wa stakabadhi mazao ghalani ambao wanaamini unamnyonya mkulima.
“Wanamtwara zao letu kuu na korosho, ambalo kwa takribani miaka 15 limetuama kwa sh. 1,200..na malipo yake yanakuwa nusunusu tena wanatukopa..mimi niwaahidi kwa kushirikiana na Mhe. Edward Ngoyai Lowassa, tukiingia madarakani tunafuta stakabadhi ghalani Mtwara..” alisema.
Aidha, mgombea huyo amewataka wananchi wa Mtwara kuandaa mdahalo utakaomkutanisha na Hasnain Murji, ili wananchi waweze kuwapima na kujua nani anafaa kuwatumikia.
No comments:
Post a Comment