Shirikisho
la Mpira wa Miguu nchini Tanzania (TFF) limesaini mkataba mpya wa miaka mitatu
(3) wa udhamini wa Ligi Kuu Tanzania bara (VPL) wenye thamani ya shilingi
bilioni sita (tsh bilioni 6.6) na kampuni ya simu ya Vodacom, halfa hiyo imefanyika
leo katika ofisi za makao makuu ya kampuni hiyo eneo la Mlimani City jijini Dar
es salaam.
Akiongea
wakati wa kusaini mktaba huo mpya, Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya simu ya
Vodacom Kelvin Twissa, amesema kampuni yao inafurahia kuendelea kuwa sehemu ya udhamini
ya ligi kuu nchini, mafanikio ya timu bora na kufanya vizuri katika michuano ya
kimataifa inatokana na kuwa na ligi bora ambayo inadhaminiwa na Vodacom.
Naye
Rais wa TFF, Jamal Malinzi amewashukuru kampuni ya Vodacom kwa kukubali
kuendelea kuidhamini ligi kuu kwa kipindi kingine cha miaka mitatu (3) na
kuongeza sehemuya udhamini wao kwa asilimia 40%.
"Tunaishukuru
kampuni ya Vodacom kwa kuendelea kuwa sehemu ya mafanikio ya mpira wa miguu
nchini, udhamini wanaotupatia unavisaidia vilabu kujiandaa na kujiendesha na
mikikimikiki ya ligi na kuifanya ligi kuwa na ushindani wa hali ya juu, msimu
huu ligi itakua na timu 16 tunatarajia kuendelea kushuhudia uhondo huo chini ya
udhamini wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom". alisema.
Mkataba
huo mpya wa udhamini kwa kipindi cha miaka mitatu, umeboreshwa na kuwa na
ongezeko la asilimia 40% kutoka katika mkataba wa awali uliomalizika.
Ligi
Kuu ya Vodacom inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 12, 2015.
SOURCE: TFF
No comments:
Post a Comment