Mwili wa marehemu Clara Mwatuka ukiwa katika jeneza ukipelekwa kaburini kwa ajili ya kuzikwa, kijijini kwao Nanganga, Masasi, mkoani Mtwara. |
Mwili wa marehemu Clara Mwatuka, ukiwa ndani ya jeneza kwa ajili ya kuagwa kabla ya kwenda kuzikwa. |
Jeneza lililo na mwili wa marehemu Clara Mwatuka, likielekea kuingizwa kaburini. |
Wananchi na baadhi ya viongozi wa serikali wakiuzika mwili wa Clara Mwatuka. |
Aliyekuwa mbunge wa Nanyumbu Dastan Mkapa, akiweka shada juu ya kaburi la Clara Mwatuka. kwa mbali ni mbunge wa Mtwara mjini anayemaliza muda wake Hasnain Murji, naye akielekea kuweka shada. |
Na Juma Mohamed, Masasi
HATIMAYE
mwili wa aliyekuwa mbunge wa viti maalumu kupitia Chama cha Wananchi (CUF),
Clara Mwatuka, umezikwa kijijini kwao Nanganga , wilayani Masasi, mokani Mtwara
jana huku mamia ya wakaazi wa kijijini hapo wakiangua vilio kwa kuondokewa na
mpendwa wao.
Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai, alisema
kifo cha mbunge huyo sio tu pigo kwa bunge bali ni pigo pia kwa wananchi wa
mikoa ya Lindi na Mtwara kutokana na namna ambavyo alikuwa akitetea masilahi ya
wananchi hao katika vikao vya bunge.
“Hakuwasahau
ndugu zangu, aliwasemea sana bungeni..naamini kabisa ameacha mfano bora na
alituelimisha kwa mambo mengi mengi ya kuwatetea..kwahiyo niahidi hapa kwamba
baadhi ya haki zake tutazifuatilia na kuzishughulikia zile ambazo zimebakia kule..”
alisema Ndugai.
Aidha,
aliongeza kuwa ofisi ya bunge itatoa fedha sh. Milioni tano huku shirika la
bima la Jubilee Insurance ambalo linashughulikia maswala ya Bima kwa wabunge
ikiwa ni pamoja na Bima za ajali, litatoa kiasi kama hicho cha fedha kwa
familia ya marehemu, ikiwa ni pamoja na kumuuguza mume wa marehemu ambaye bado
yuko hospitalini.
Makamu mwenyekiti
wa Chama cha Wabunge Wanawake, Mhe. Suzan Lyimo, akizungumza kwa niaba ya
mwenyekiti wa chama hicho, Anna Abdallah, alisema wao kama chama wamechangia
kiasi cha sh. Milioni 1 huku katibu wake bado akiendelea kuchangisha na kiasi
kitakachopatikana kitatolewa kwa familia hiyo.
No comments:
Post a Comment