Mwandishi na mtangazaji wa redio Pride ya mkoani Mtwara, Andrew Mtuli, akizungumza jambo katika kikao cha pamoja cha waandishi wa habari na viongozi wa vyama vitatu kati ya vinne vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kilichoitishwa na Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mtwara (MTPC) juzi, kutaka muafaka juu ya jimbo la Mtwara mjini baada ya kuwa na mvutano baina ya vyama hivyo mkoani Mtwara. |
Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi mkoa wa Mtwara, Uledi Hassan akizungumza jambo katika kikao cha pamoja na waandishi wa habari kilichoitishwa na Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mtwara (MTPC) juzi, kutaka muafaka juu ya jimbo la Mtwara mjini baada ya kuwa na mvutano baina ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) mkoani Mtwara. |
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoa wa Mtwara, Willy Mkapa, akizungumza jambo katika kikao cha pamoja na waandishi wa habari kilichoitishwa na Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mtwara (MTPC) juzi, kutaka muafaka juu ya jimbo la Mtwara mjini baada ya kuwa na mvutano baina ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) mkoani Mtwara. |
Mkurugenzi wa siasa wa Chama cha Wananchi (CUF) mkoa wa Mtwara, Saidi Mtunduima, akizungumza jambo katika kikao cha pamoja na waandishi wa habari kilichoitishwa na Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mtwara (MTPC) juzi, kutaka muafaka juu ya jimbo la Mtwara mjini baada ya kuwa na mvutano baina ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) mkoani Mtwara |
Na Juma
Mohamed, Mtwara.
CHAMA cha
Waaandishi wa Habari Mkoa wa Mtwara (MTPC) kimefanikiwa kuwakutanisha na kumaliza
mvutano ulikuwepo awali juu ya chama gani kimepewa ridhaa ya kusimamisha
mgombea ubunge katika jimbo la Mtwara mjini na Umoja wa Katiba ya Wananchi
(UKAWA).
Hatua hiyo
imekuja baada ya kikao cha pamoja kilichafanyika juzi kati ya viongozi wa vyama
vitatu ambavyo vilikuwa na mvutano ambavyo ni NCCR-Mageuzi, Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Chama cha Wananchi (CUF), na waandishi wa
habari wa mkoani hapa.
Kikao hicho
kilichoitishwa na uongozi wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mtwara
(MTPC), kilikuwa na lengo la kupata kauli ya pamoja juu ya nani aliehidhinishwa
na UKAWA kusimamisha mgombea, baada ya kuona baadhi ya viongozi wa vyama vya
siasa na wafuasi wao kuanza vitisho kwa waandishi na wengine kwenda redioni
kujinadi kuwa wao ndio wamepewa jimbo hilo.
Akizungumza kwa
niaba ya waandishi wengine, mwandishi na mtangazaji wa Redio Pride ya mkoani
hapa, Andrew Mtuli, alisema kumekuwa na mazingira magumu kwa waandishi katika
kipindi hiki ambacho bado kumekuwa na mvutano juu ya nani aliyepewa jimbo na
UKAWA, kutokana na kila chama hasa vyama viwili vya NCCR na CUF kujinadi kila
kimoja kwa madai kuwa kimeidhinishwa na umoja huo kusimamisha mgombea.
“Bado kila
mtu hamuamini mwenzake kwamba yeye ndio amepewa fursa ya kusimamisha mgombea, kwahiyo
mtu wa CUF akisema kuwa sisi ndio tumepewa fursa alafu ukasema redioni, unapata
shida kwa mtu wa Chadema, ukisema mtu wa Chadema ndio amepewa hiyo fursa baada
ya kumnukuu mtu wa juu ambaye sisi waandishi ndio tuna ‘balance’ kutoka kwake
unapata shida kwa mtu NCCR, na hivyo hivyo kwa mtu wa NCCR..” alisema.
Alisema waandishi
walianza kupata ujumbe wa vitisho kutoka kwa badhi ya wafuasi wa vyama hivyo
baada ya viongozi wao kwenda redioni kwa nyakati tofauti kila chama kuzungumza
juu ya jimbo hilo kupewa na UKAWA.
Aidha, baada
ya kupewa nafasi ya kuzungumza kila kiongozi wa chama katika kikao hicho, mwanzoni
mwenyekiti wa NCCR mkoa wa Mtwara, Uledi Hassan, ambaye anagombea ubunge katika
jimbo hilo alisema kuwa jimbo hilo wamepewa wao kutokana na makubaliano
yaliyofikiwa katika kikao cha Agosti 17 mwaka huu kilichofanyika Kawe, Dar es
Salaam kati ya viongozi watau wa UKAWA ambao aliwataja kwa majina kuwa ni James
Mbatia (NCCR), Emmanuel Makaidi (NLD) na Twaha Kasilima akiwakilisha (CUF).
“Nimetoa tarehe,
nimetoa mpaka ukumbi na idadi ya watu waliokaa ili mujiridhishe na haya
ninayosema..sasa hizi siasa kila mtu ana ‘interest’ zake, labda kuna watu
wengine hawakupenda jimbo hili kupewa Uledi..” alisema.
Mkurugenzi wa
siasa wa CUF mkoa wa Mtwara, Saidi Mtunduima, alisema kigezo kimoja wapo
kinachotumika na UKAWA kugawa majimbo kuangalia chama chenye mtaji mkubwa,
ambapo alisema CUF kina mtaji mkubwa Mtwara na hivyo kupewa jimbo hilo huku
akionyesha baruwa iliyosainiwa na Naibu Mkurugenzi wa Uchaguzi na Mipango wa
chama hicho, Shaweji Mketo, kutoa ridhaa ya kuchukuwa fomu kwa mgombea wa CUF.
Naye, katibu
wa Chadema mkoa wa Mtwara, Willy Mkapa, alisema waliamua kusimamisha mgombea
katika jimbo hilo kutokana na kutopata waraka wowote ulioidhinisha kuwa chama
gani kinapaswa kusimamisha mgombea, na hivyo kuamini kuwa bado jimbo hilo
hakijapewa chama chochote huku akiwataka viongozi wakuu wa UKAWA kutuma waraka
rasmi kama walivyofanya katika ngazi ya udiwani ili kuondoa mgogoro na sio
kuzungumza kwa simu.
Baada ya
kauli hizo, Mtuli aliwataka viongozi hao kuwasiliana na viongozi wa juu ili
kuwaomba watoe waraka ambao utasainiwa na viongozi wa vyama vyote vya UKAWA
ambao utaondoa utata uliopo na kuwafanya waandishi wa habari kufanya kazi kwa
uhuru, jambo ambalo liliungwa mkono na viongozi wote kwa pamoja na kutoka na
kauli moja kwamba UKAWA bado hawajatoa idhini kwa chama chochote kusimamisha
mgombea katika jimbo hilo.
Akizungumza kwa
niaba ya viongozi wengine, Uledi Hassan, aliwashukuru waandishi wa habari na
uongozi wao kwa kuamua kukutananao ili kuweza kutafuta muafaka wa jambo hilo.
“Nafikiri
kama mungefanya hivi tokea mara ya kwanza labda hapa tulipo tusingefikia..sasa
binafsi nimefarijika na kwaniaba ya wenzangu wote niseme tunawashukuru sana na
bado tuendelee kuwa karibu katika hiki na kile..” alisema.
No comments:
Post a Comment