Na Juma
Mohamed, Lindi.
Kamanda wa
vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Lindi na aliyekuwa mgombea Ubunge
kupitia chama hicho jimbo la Mtama, mkoani Lindi, Selemani Methew amesema
hayuko tayari kuona haki yake inaporwa na viongozi wachache ndani ya chama
hicho kwa masilahi yao binafsi.
Aliseema
kura za maoni zilizofanyika ktika jimbo la mtama viongozi wa CCM wilaya
hawakutenda haki walitumia nguvu, vitisho, wizi wa kura na hata rushwa
kuhakikisha mgombea waliomtaka anashinda.
Hayo
aliyazungumza juzi katika mkutano wa hadhara uliyofanyika katika viwanja vya
sokoni jimboni humo ambapo alitumia fursa hiyo kumshukuru waziri mkuu Mh
Mizengo Pinda na mkuu wa mkoa wa Lindi Mwantumu Mahiza, ambao walimshauri kuwa
na subira baada ya kuwasilisha malalamiko yake ofisi za CCM taifa, ili kikao
cha kamati kuu kiweze kuamua nani anastaili kusimama kwenye jimbo hilo.
Alisema
hali hiyo inaonyesha jinsi gani chama hicho kinavyoharibiwa na wana-CCM
wachache wasiokuwa wazalendo, na wenye tamaa na uchu wa madaraka,wasiotaka
kutenda haki wala kufuata mifumo ya uongozi.
Methew alitumia
mkutano huo wa hadhara kuwaomba wapambe wake kumuunga mkono endapo jina lake
halitarudi CCM wawe tayari kumuunga mkono kokote atakapokwenda jambo ambalo
liliungwa mkono na mamia ya wanachama na wananchi waliokuwa katika mkutano huo.
“maadui
zangu wanaodhani joto la kukubalika liko mtama mjini wanajidanganya,
nitakachokifanya kwa sasa ni kufanya ziara ya kata kwa kata kuwashukuru
wananchi walionipa kura katika uchaguzi wa kura za maoni ccm -hivyo nawaoma
ndugu zangutuungane muone uungwaji mkono wangu katika maeneo hayo”.alisema.
Alisema
alilazimika kurudi mtama baada ya kuitwa na wazee wa mji akitokea jijini Dar Es
Salama ambapo aliondoka kwa minajili ya kuwasilisha malalamiko yake baada ya
kutordhia matokeo ya kura zamaoni ambapo alipata elfu nne na kuwa wa pili
dhidi ya Nape Nnauye aliyepata kura elfu tisa.
Akijibu
tuhuma hizo ambazo nyingi zimeelekezwa kwenye ofisi yake katibu wa ccm
wilaya ya Lindi vijijini Christina Gukwi, alisema Nape alishinda kihalali na
tuhuma hizo ni malalamiko ya mtu aliyekosa kura na kwenye siasa ni jambo la
kawaida.
Akizungumzia
wizi wa kura amesema jimbo la mtama lina kata zipatazo 20 matawi Zaidi ya
miamoja hivyo katika hali ya kawaida si jambo raisi kuiba kura kama
wanavyofikiria na kitu hicho hakipo, na kuongeza kuwa katika mkutano huo
alituma watu wa ofisi yake ambao wamerokodi kila kitu kilichoongelewa katika
mkutano huo.
Kwa upande
wa wananchi kulingana na mapenzi waliyokuwa nayo walilazimika kuchangishana na
kukodi magari kwa ajili ya kumpokea mpendwa wao maandamano yaliyoanzia eneo la
Mnazimmoja ikiwa ni kilometa 30 kufika jimbo la mtama mjini.
Wakizungumza
kwa jazba baadhi ya wakereketwa wa chama hicho akiwamo Ali
Matoroka alisema
uchaguzi huo umeleta mpasuko na kusababisha makundi kati ya kundi la Nape na
Selemani Methew ambao kila siku wamekuwa wakipelekeana polisi kutokana na
chokochoko zisizo isha na wamba hali kama itaendelea hivyo watashindwa
kuzikana.
Naye
katibu wa UWT tawi la Mihogoni aliyepewa nafasi ya kuzungumza katika jukwaa
alisema wanasikitishwa na kitendo cha kuibiwa kura kulikofanywa na baadhi ya
viongozi wa CCM hivyo kumtaka aende kokote wako nyuma yake.
No comments:
Post a Comment