Mgombea ubunge jimbo la Mtwara mjini kupitia chama cha NCCR-Mageuzi, Hassan Uledi. |
Na Juma
Mohamed, Mtwara.
MGOMBEA
Ubunge jimbo la Mtwara mjini kupitia chama cha NCCR-Mageuzi, Hassan Uledi, amekiri kuwa bado jimbo hilo lipo katika hali
ya sintofahamu juu ya nani anapaswa kuwa mgombea rasmi kupitia vyama
vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).
Uledi aliyazungumza hayo mapema leo baada ya kuchukuwa fomu ya kugombea ubunge kwa jimbo hilo, katika ofisi ya mkurugenzi wa manispaa ya Mtwara Mikindani, Limbakisye Shimwela.
Kumekuwa na
mvutano mkubwa kwa vyama viwili vya NCCR-Mageuzi na Chama cha Wananchi (CUF)
kati ya vinne vinavyounda UKAWA juu ya chama gani kinachopaswa kusimamisha
mgombea katika jimbo hilo.
Alisema, aliitwa na viongozi wa UKAWA akiwa na mgombea wa CUF, Maftaha Nachuma
ambaye tayari amechukuwa fomu, na kukutanishwa na mwanasheria ambapo walihojiwa
juu ya nani anayefaa kugombea jimbo hilo lakini bado hakukuwa na maamuzi
yaliyotolewa kuamua nani anafaa kugombea.
“Kwahiyo
kwakuwa chama changu kinakwenda na wakati, wameniamrisha nichukue fomu leo ili
hapo itakapotamkwa kuwa ni nani asimame, iwe tayari nimeshajipanga kwa kila
jambo..” alisema.
Aliwataka
Wanamtwara kukumbuka historia ya matukio yaliyotokea awali wakati wa vurugu za
gesi na kuepuka kuwaunga mkono watu ambao wanajitokeza katika kipindi hiki
ambacho hali imetulia na kuwaaminisha kuwa wao ndio wanafaa kuwa wawakilishi
wao bungeni.
No comments:
Post a Comment