Friday, August 21, 2015

Mafanikio mitambo ya Madimba yaanza kuonekana baada ya Mnara kuwaka moto



Mnara wa usalama ulio katika kiwanda cha kuchakata gesi kilichopo Madimba, mkoani Mtwara ambao unawaka kuashiria kuimarika kwa mitambo kiwandani hapo pamoja na mabomba kutokuwa na hitirafu


Muonekano wa kiwanda cha kuchakata gesi asilia, Madimba mkoani Mtwara.


Kiwanda cha kuchakata gesi asilia, Madimba Mtwara.


Meneja Mradi wa ujenzi wa bomba la gesi na kiwanda cha kuchakata gesi, Madimba, Mtwara, Leonce Mrosso




Na Juma Mohamed, Mtwara.

Hali ya usalama katika mitambo ya kuchakata gesi asilia katika kiwanda cha Madimba mkoani hapa imeimarika kutokana na mafanikio yaliyoonekana baada ya gesi kufika katika mitambo hiyo kutoka katika kisima cha (MB 3) kilichopo Mnazibay, Msimbati.

Akizungumza na mtandao huu hii leo, Meneja Mradi katika kiwanda hicho, Leonce Mrosso, alisema mafanikio ya ubora wa mitambo hiyo yameonekana kutokana na kuwaka moto katika mnara maalumu ulio kando ya kiwanda hicho ambao unaunguza gesi ambayo haitakiwi kusafiri katika bomba (Flash Gas)


Alisema kwa sasa hatua iliyopo baada ya kufanikisha kuifikisha gesi kiwandani hapo, ni majaribio ya mitambo, zoezi linalofanyika kwa wiki mbili kabla ya kuanza kuisukuma kwenye bomba kubwa linalotoka kiwandani hapo hadi Kinyerzi, Dar es Salaam ambapo itakuwa ni kati ya Septemba 10-15 mwaka huu.

No comments: